Huwezi amini huyu jamaa kwa jina anaitwa Jumanne Juma, lakini hebu mcheki anavyojisevia chai asubuhi na mapema bila aibu, wala kufuata basi taratibu za dini angalau kujificha wakati akila mchana katika mwezi mtukufu kama huu.
Wapo wengi kama huyu jamaa ambao wengi wao unapowauliza kulikoni basi jibu ni jepesi tu ''Nina matatizo ya vidonda vya tumbo'', hivyo vidonda vya tumbo mbona hatujawahi kukusikia ukilalamika kabla ya kuanza kwa mwezi mtukufu? ''Acheni kumkufuru mungu kwa kumuomba maradhi msiyokuwa nayo na pindi atakapowapatia mtakuwa mkisingizia nini? hivi tu hamna na mnasingia vidonda vya tumbo je mkiwa na hivyo vidonda si mtananiliu na kina naniliu wenu mchana kweupe msingizie mnaumwa?
Huyu naye ni Al-maarufu kama Kambi Mbwana.... tena jina la wenyewe huko kwa wanaoelewa maana halisi ya mfungo wa mwezi huu, lakini akaaaaaaaa!!!!! ni kama hajui kuwa kuwa hastaili kula mahala hapa tena mchana kweupe na mbele za watu wanaomfahamu.
Mwenyezi Mungu katika maandiko yake matakatifu amewaharalishia kula mchana Kina Mama wenye matatizo ya kina mama. ujauzito, kunyonyesha, tena kwa wanaonyonyesha na wajawazito nao pia ni kama hawajiwezi na kuambiwa kuwa kama wataweza wameruhusiwa kufunga wawezavyo na kulipa walizoacha na yule aliyea katika magonjwa ya kina mama lakini naye pia atalipia atakapopona. Je vipi mwenzetu utalipia lini????
kwelikakanguwatu wanafanya vibaya kabisa hii ya kula mchana kweupe tena mijanaume mizima. Kama ni kweli mwenyezi mungu awasamehe ana kama wanadanganya pia Mungu ndie anayejua kwani hawamdanganyi binadaam yeyote na wanadanganya nafsi zao.
ReplyDelete