Habari za Punde

*WADAU JITOKEZENI KUUINUA MCHEZO WA PIKIPIKI TANZANIA

 Mwendesha Pikipiki wa Kinondoni, Msawila Mahonda, akionyesha uwezo wake wa kuchezea Pikipiki, wakati wa mazoezi yao ya kila siku ya Jumapili kwenye Viwanja vya Tanganyika Pakers, Kawe jijini Dar es Salaam. 

Pamoja na waendesha Pikipiki hao kujitahidi kutengeneza njia na uwanja wa mchezo huo katika eneo hilo kwa kujitolea na kuwafanya mashabiki lukuki wa mchezo huo kukusanyika kila siku ya jumapili ili kupata burudani, lakini bado mchezo huo haupewi 'Sapoti' ya kutosha na wadau wa michezo nchini na Wizara husika kama ambavyo inaonekana katika michezo mingine kama ulivyo chezo wa Soka ambao kila kukicha wanajitokeza wadhamini wa mchezo huo na kumwaga 'Mihela' mingi kwa kupromoti jambo ambalo tayari limekwishapita katika hatua hiyo likisubiri hatua nyingine. 

Picha inayofuata ni mwendesha Pikipiki wa nje.
 Kwa wenzetu wanaojua nini maana ya michezo huandaa kama hivi, njia za pikipiki njia nzima ikia na alama za kuwaongoza madereva pindi wanapokuwa mchezoni.
 Kwa wenzetu hata uwanja unakuwa umeandaliwa kama hivi, na wale wanaopenda michezo hujitangaza kupitia mchezo huo kama inavyoonekana pichani mabango kibao ya matangazo.
 Hapa mpiga picha aliyepiga picha hii hakukusudia kupata shoti iliyobora tu ya mwendesha pikipiki huyu, bali alikusudia na 'Back Ground' ya watu na matangazo yanayoonekana picha kuashiria mvuto wa mchezo huu.
 Hata picha ikipigwa kwa mbali lakini bado kilichopo uwanjani hapo hakiongopi kitaonekana tu kuwa ni mashabiki lukuki wa mchezo huu na matangazo ya biashara.
 Kwenye Uwanja wetu wa Tanganyika Parkers Kawe kamwe hutamkuta Rider akicheza kama hivi, si kama hawawezi la hasha ila mazingira ya uwanja hayaruhusu, ''tuwasapoti ili tuone uwezo wao''
 Hebu ona hizi njia zilivyoandaliwa. Sidhani kama kweli hawapo wadau wenye uwezo wa kujitolea kufanya kama hivi ili kuuendeleza mchezo huu.
 Rider, anafanya atakavyo kutokana na kuandaliwa kwa njia nzuri.
 Si kwamba Pikipiki inamuendesha, hapana yeye ndiye anaiendesha Pikipiki, yote haya yanawezekana tukiwa na nia na pia tutawavutia hata majirani zetu, kama imewezekana kujengwa Uwanja wa Soka wa kisasa itashindikanaje Uwanja wa mchezo huu pendwa?.
 Hizi zote ni burudani hadi wewe mshabiki unavutiwa kufika ili kujionea live, kama ilivyo kwa Kawe lakini haipatikani raha kamili kutokana na ubovu wa maeneo.
 Action hii na tangazo lililo nyuma ya picha hii unazani Kampuni hii imejitangaza kwa kiasi gani?.
 Hebu ona njia hizi chini (kulia).....
 Kutokana na kuandaliwa kwa njia kama hivi ndiyo siri ya Rider huyu anayeonekana yu hewani zaidi.
 Yote haya ni machejo tu, hapa chini yake ndipo ilipo njia yenye tuta kubwa.
 Haya anaweza kuyafanya Rider Mbongo maarufu kama Ludan Volvo, akiwezeshwa.
Hebu sasa tujionee viwanja vyetu vya Kawe pamoja na mashine wanazotumia Marider wetu.
 Huyu ni Msawila akiruka tuta...Kawe Dar es Salaam.
 Marider, Dotto (nyuma) na Msawila, wakichuana wakati wa mazoeziyao Kawe...
 Mchuano wa Dotto na Msawila unaendelea......
 Mchuano unaendea.......
 Hapa wote wakilala lwenye kona ambayo haina alama yeyote na pembeni kama inavyoonekana pembeni ikiwa imeegeshwa Pikipiki isiyohusiana na mchezo huo jambo ambalo ni hatari.
 Rashidi Kiparacha, akiruka tuta....
 Rashidi Kiparacha akiendelea kujifua....
 Kutokana na ubovu wa uwanja huo usio na maandalizi ya kutosha umesababisha Rashid Kiparacha kujikuta akiuvaa msitu huu wenye miba baada ya pikipiki yake kugoma ghafla kushika breki.
Makofia akionyesha uwezo wa kupita katika mabonde.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.