Habari za Punde

*WFP NA WIZARA YA KILIMO WASAINIANA MKATABA WA MAKUBALIANO YA UNUNUZI WA MAHINDI YA VIKUNDI VYA WAKULIMA

 Richard  Ragan (kulia) akipeana mkono na  Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza(kushoto wa pili)  jana jioni (juzi) mjini Dodoma mara baada ya utiaji saini wa makubaliano ya ushirikiano wa ununuzi wa  mahindi  kutoka kwa vikundi vya wakulima wenye lengo la kupanua masoko kwa wakulima. Pia   Chakula hicho kitawanufaisha  watu milioni nane wanaokabiliwa na uhaba wa chakula  kwa msaada wa WFP katika nchi za Afrika kipindi cha mwaka 2012/ 2013. Kushoto ni  Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ,  Mohamed Muya na wa (pili kulia) ni  Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa .Picha  na Magreth Kinabo, MAELEZO.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika ,  Mohamed Muya(kushoto), Mtendaji  Mkuu wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA) Charles Walwa na Mwakilishi Mkazi na Mkurugenzi wa Shirika la Chakula la Dunia(WFP), Richard  Ragan (kulia) wakisaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano wa ununuzi wa  mahindi  kutoka kwa vikundi vya wakulima wenye lengo la kupanua masoko kwa wakulima. Pia   Chakula hicho kitawanufaisha  watu milioni nane wanaokabiliwa na uhaba wa chakula  kwa msaada wa WFP katika nchi za Afrika kwa kipindi cha mwaka 2012/2013 . Kushoto wa pili ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Christopher Chiza akishuhudia utiaji saini huo katika Ofisi za wizara hiyo jana(juzi) mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.