Ukifika mjini Zanzibar huwezi kutembea umbali wa mita 200, bila kukutana na usafiri wa aina hii ya Ng'ombe au Punda aliyesheheni mzigo mzito huku akikokotwa na wengine huwa wamebeba mzigo pamoja na mhusika bila huruma.
Kwa kweli muda mwingine unapokutana na punda au Ng'ombe aliyebebeshwa mzigo unaweza kumuonea huruma japo si wako, wengine hubebeshwa matofali yenye uzito unaotakiwa kubebwa na Pick Up, na wengine huwabebesha magogo makubwa ya miti na mizigo mingineyo bila huruma, na ndiyo maana mtandao huu umeguswa na kuamua kuwauliza wahusia je wapo pande hizo? ili kuwanusuru wanyama hawa kiukweli.
Hapa Punda huyu akibebeshwa Madumu ya maji na pia mhusika huyu pia atapanda kwa punda huyu na madumu yake bila huruma, kama ambavyo umeona picha ya juu ni Ng'ombe akiwa amebeba mzigo pamoja na wahusika.
No comments:
Post a Comment