Habari za Punde

*KHADIJA MNOGA ATUA NA 'MGENI' MPYA AWALINGISHIA MASHABIKI WA EXTRA BONGO

Kimobitel akiimba wimbo wake alioutunga mwenyewe unaojulikana kwa jina la 'MGENI' ndani ya Meeda Sinza Usiku wa kuamkia leo.
Kulia ni Mkurugenzi wa Extra Bongo Ally Choki akiimba wimbo mpya wa Kimobitel ndani ya Meeda Sinza.
Banza Stone AKA General, akifurahi pamoja na Khadija Mnoga AKA Kimobitel wakati wa utambulisho usio rasmi wa ujio wa Kimobitel.
Athanas mwanamuziki anayekuja kwa kasi ndani ya Extra Bongo, akishoo luv na Kimobitel ndani ya Meeda Sinza.
Safu ya wanamuziki nguli wa Extra Bongo walioimba wimbo mpya wa Kimobitel (Mgeni) wakiongozwa na Ally Choki wa pili (kushoto) wa kwanza kulia ni Rogert Hega Katapila, anafuatiwa na Banza Stone na Kushoto ni Kimobitel.
Kimobitel akiwa na nyuso ya furaha baada ya wapenzi na wadau mbali mbali kumpongeza na kumpokea kwa mikono na kumkaribisha rasmi kujiunga kwa mara ya pili na bendi yake ya Extra Bongo.
 
Khadija Mnoga "Kimobitel" hivi majuzi alitangaza rasmi kuihama Bendi ya Twanga Pepeta ambayo aliitumikia kwa muda mfupi tangu alipoihama bendi yake hiyo ya Extra Bongo na hatimaye kuamua kurejea tena kwenye jukwaa la bendi yake ya zamani iliyo chini ya Mkurugenzi wake Ally Choki. 
 
Akizungumza na mwandishi wa mtandao huu, Kimobiteli alisema kuwa sababu za kuhama na kurejea jukwaa ;a Extra Bongo ni, mipango yake ambayo alikwisha ianza akiwa na bendi hiyo chini ya Ally Choki, ambayo amerejea  kuimalizia kama wimbo usemavyo wimbo aliowahi kutunga akiwa na bendi hiyo, uitwao 'MJINI MIPANGO'.
 
Kwa mujibu wa Mkurugenzi wa Extra Bongo, Ally Choki, amesema KIMO KIMO kama anavyotambulika atatambulishwa rasmi siku ya Ijumaa ya tarehe 14/09/2012 katika ukumbi wao wa nyumbani New White House uliopo Kimara Korogwe jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.