Habari za Punde

*KUNDI LA MIZENGWE LASHEREHESHA WIKI YA NENDA KWA USALAMA KITAIFA MKOANI IRINGA

 Msanii wa Kundi la Vichekesho 'MIZENGWE' , Mkwere, akiigiza kama Askari wa Usalama wa Barabarani akisimamisha magari wakati wakitoa burudani katika Uzinduzi wa Wiki ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa leo mjini Iringa katika Uwanja wa Samora. Maadhimisho hayo yameanza leo . Kaulimbiu ya maadhimisho ya mwaka huu ni “PAMBANA NA AJALI ZA BARABARANI KWA VITENDO, ZINGATIA SHERIA”.
 Mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani. Dk. Emmanuel Nchimbi akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa, Salim Ahmed Jabri Sasi, baada ya Waziri kuwsili uwanja wa Samora Iringa.
 Waziri Nchimbi akisalaimMbunge wa Viti Maalum, Rita Moto Kabati na viongozi wengine wa Mkoa wa Iringa.
 Meneja Uhusiano wa Airtel Tanzania, Jackson Mbando (kushoto) akimkabidhi Moderm ya Airtel 3.75G Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk. Emmanuel Nchimbi wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo ya Simu ambao ni wadha,mini wa Wiki ya Nenda kwa Usalama Kitaifa inayofanyika mkoani Iringa. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani na Mwenyekiti wa Baraza la Usalama Barabarani. Pereira Silima (wapili kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Dk. Christine Ishengoma. Maadhimisho ya Wiki ya Nenda kwa Usalama yameanza leo kitaifa Mkoani Iringa.
 Mkaguzi wa Polisi, Abel Swai Kutoka Trafiki Makao Makuu jijini Dar es Salaam akitoa maelezo ya namna ajali za barabarani zinaweza kuepukika endapo watumiaji wa barabara watakuwa waangalifu na kufuata sheria za barabarani. Kulia ni Waziri wa Mambo ya Ndani, Dk Emmanuel Nchimbi.
 Baadhi ya walemavu wakiingia uwanjani katika uwanja wa Samora mjini Iringa katika Uzinduzi wa Wiki ya kitaifa ya Nenda kwa Usalama iliyozinduliwa jana mjini hapa huku Kampuni ya Simu za Mkononi ya Airtel ikiwa mdhamini mkuu.
 Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia maadhimisho hayo.
 Kamnada wa Kikosi cha Polisi Usalkama Barabarani, Mohamed Mpinga, ambaye pia ni Katiraza la Usalama Barabarani, akizungumza.
 Wanafunzi wakipatiwa maelezo ya matumizi yaa yasiyo sababisha ajali.
Bendi ya Polisi Jazz ya jijini Dar es Salaam, ikitoa burudani.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.