Habari za Punde

*POLISI ZANZIBAR WAWADHIBITI VIJANA WALIOJIKUSANYA KUFANYA VURUGU KITUO CHA KUPIGIA KURA CHA BUBUBU


 Kumekuwa na vurugu za hapa na pale, Polisi kupambana na vijana kwenye kituo cha kupigia kura wakati wa  uchaguzi mdogo kumchagua Mwakilishi wa jimbo la Bububu Zanzibar jana jioni. (pichani) Polisi wa kuzuia ghasia wakisaidiwa na kikosi cha Valantia  kuwaondoa vijana   waliojikusanya karibu na kituo cha kupigia kura  kwenye  Shule ya Bububu.
Askari wakijiweka sawa kulinda amani eneo hilo.
Askari akimdhibiti mmoja wa vijana waliokuwa wakishinikiza vurugu eneo hilo.
Askari akijaribu kuwaelekeza baadhi ya vijana utaratibu unaostahili katika eneo hilo baada ya kumaliza kupiga kura ili kusubiri matokeo.
Baadhi ya vijana wakihamaki, baada ya kuona askari wakiwasili eneo hilo na kuanza kuwatawanya.
Askari wakishushwa katika gari wakati wakiwasili katika eneo lililokuwa na vurugu ili kudhibiti vurugu hiyo iliyokuwa imeandaliwa na baadhi ya vijana, waliokiwa wakipinga matokeo.

 Baadhi ya mawakala wa vyama wakifuatilia upigaji kura.


 Kijana akitumbukiza kura yake kwenye kisanduku cha kupigia kura kwenye moja ya kituo cha Shule ya Bububu Zanzibar.

Kiongozi wa chama cha siasa (kushoto) akizungumza na wandishi wa habari nje ya kituo cha kupigia kura. Picha zote na Martin Kabemba.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.