Habari za Punde

*REDDS MISS KINONDONI APATIKANA USIKU WA KUAMKIA LEO




Mshindi wa shindano la Redds Miss Kinondoni Brigit Alfred, akiwapungia mkono mashabiki walioshuhudia shindano hilo jijini Dar es Salaam jana, kulia ni mshindi wa pili Diana George Hussein na mshindi watatu Irene David.
 Warembo hao wakiwa kwenye vazi la ufukweni wakipita mbele ya majaji na watazamaji walioshuhudia shindano hilo.
 Mshindi aliyenyakua taji hilo Brigit Alfred akicheza midundo ya kihindi kwenye kinyang'anyiro cha vipaji na kuibuka kidedea.
Hawa ndio waliofika tano bora kutoka kushoto ni, Judith Sangu, Brigit Alfred, Diana George Hussein, Irene David na Kudra Lupatu.
Redds miss Kinondoni anayemaliza mudawake Stela Mbugi, akiwa kwenye picha yapamoja na tanobora kabla ya kukabidhi taji hilo.
 Brigit Alfred akipungia mashabiki mara tu baada ya kutangazwa kua mshindi wa shindano hilo.
Judith Sangu akionyesha uwezo wake wa kucheza muziki kwenye Miss Tallent.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.