Na Mwandishi Wetu, Jijini Dar
Serikali imesema itatumia shs 30 bilioni kukamilisha ujenzi wa mkongo wa taifa na kurahisisha huduma hiyo hapa nchini.
Hayo yalisemwa na Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Technolijia, Makame Mbarawa wakati wa ufunguzi wa mkutano wa sita wa wadau wa mawasiliano duniani (Capacity Africa) uliodhaminiwa na kampuni ya Six Telecoms ambao umefanyika Tanzania kwa mara ya kwanza kwa siku mbili.
Waziri wa mawasiliano, Sayansi na Technolijia, Makame Mbarawa |
Mbarawa alisema ujenzi huo huko kwenye awamu ya pili huku km 7560 zikiwa zimemalizika kuunganishwa na tayari zimeanza kutumika kwenye makao makuu ya mikoa yote nchini na tayari kampuni sita kutoka Rwanda, mbili za Malawi, mbili za Zambia na mbili za Burundi zimeomba kuunganishwa kwenye mkongo wa taifa," alisema Mbarawa katika mkutano huo.
Mkutano huo uliondaliwa na kampuni ya Six Telecoms umewakutanisha wadau wa mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50 duniani ulilenga pia kuitumia Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi nane za Afrika.
Mkurugenzi mkuu wa kampuni ya Six Telecoms, Rashid Shamte alisema ujio wa mkongo wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kwenye sekta hiyo.
Shamte alisema lengo la mkutano huo ni kuitumia Tanzania kuwa njia ya mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na kuongeza kwamba hiyo itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya mawasiliano hapa nchini.
Alisema kuwa wamefarika sana kufanikisha mkutano huo na kutambulisha mtandao wao wa Metro ambao unaongoza katika soko kwa hivi sasa.
Kwa mujibu wa Shamte, pamoja na changamoto kadhaa wanazokabiliana nazo, wameweza kujidhatiti ili kuweza kufikia lengo lao hapa nchini na katika makampuni mengine nje ya Tanzania yanayotumia huduma yao.
“Ninafuraha kubwa kuona mkutano huu wa Capacity Africa unafanyika hapa nchini na mwitikio kuwa mkubwa, kwa kweli hii ni faraja sana kwetu, najua mkutano huu utatoa picha ya nini kitafanyika ili kukabiliana na changamoto ambazo watumiaji wa huduma zetu wanakabiliana nazo, naipongeza serikali kwa kutoa sapoti kubwa na wadau wote duniani kukutana na hili ni kwa ajili ya kujenga na kuleta maendeleo katika nchi zetu,” alisema Shamte.
Wadau wa mawasiliano zaidi ya 350 kutoka nchi 50 duniani ulilenga pia kuitumia Tanzania kuwa njia kuu ya mawasiliano kwa nchi nane za Afrika. Shamte alisema ujio wa mkongo wa taifa utawavutia zaidi wawekezaji kuja Tanzania kuwekeza kwenye sekta hiyo.
Alisema kuwa lengo la mkutano huo ni kuitumia Tanzania kuwa njia ya mawasiliano kwa nchi nane ilizopakana nazo na kuongeza kwamba hiyo itasaidia pia kupunguza gharama kwa watumiaji wa sekta ya mawasiliano hapa nchini.
Wadau wengine waliodhulia mkutano huo ni wawakilishi kutokaLiquid Telecom, WIOCC, Safaricom Business, Seacom, Gateway na kampuni mbalimbali za mawasiliano duniani.
No comments:
Post a Comment