Habari za Punde

*WAFANYABIASHARA WA UINGIZAJI NA USAFIRISHAJI MADAWA KUTOKA CHINA NA TZ WAKUTANA DAR

Makamu wa Rais wa chama cha wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji wa dawa na vifaa tiba kutoka China (CCCMHPIE)  Meng Dongping, akizungumza katka mkutano wa wafanyabiashara wa Uingizaji na Usafirishaji wa bidhaa hizo kutoka nchini China Uliofanyika leo jijini Dar es Salaam. Amesema Tanzania ni nchi ya 11 katika ushirikiano wa kibiashara wa bidhaa hizo barani Afrika na nchi ya pili kwenye soko la bidhaa hizo wa nchi za EAC. ambapo katika kipindi cha miezi 6 cha mwaka 2012 ukuaji wa soko la bidhaa hizo nchini Tanzania umefikia dola za Marekani milioni 32.61 sawa na asilimia 47. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
 Mdau  wa mkutano huo kutoka (MSD ) nchini, Cosmas Mwaifani, akiwasilisha mada yake katika mkutano huo wa siku moja jijini Dar es Salaam.
 Baadhi ya washiriki wa mkutano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki  wa kuleta dawa na vifaa tiba kutoka kwa wafanyabiashara wa uingizaji na usafirishaji wa  madawa na  vifaa tiba kutoka China  wakifuatilia mada mbalimbali katika mkutano huo wa siku moja jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.