NA MAGRETH KINABO
BODI ya Utalii Tanzania, imeandaa mpango maalum kwa kutangaza utalii wa kiutamaduni, kwa kutumia filamu itakayoonesha vyakula vya kiasili vya Kitanzania kushirikiana na mpishi maarufu duniani kutoka nchini India, Sanjeev Kapoor.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo, Alyce Nzuki wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye hoteli ya Serena iliyopo jijini Dares salaam.
“Bodi ya utalii Tanzania imeona ni fursa kutangaza utalii wa kiutamaduni kwa kumtumia mpishi huyu maarufu ambaye atatengeneza filamu ya kuonesha utalii wa kiutamaduni kwa kutumia vyakula vya Kitanzania.
Filamu hii itaorushwa katika runinga yake ya ‘Food Food Channel’,” alisema Nzuki.
Nzuki aliongeza kuwa filamu hiyo itaoneshwa nchini India na duniani kote hususan Asia hivyo itasaidia kukuza utalii na kukuongeza idadi ya watalii nchini.
Naye mpishi huyo, Kapoor alisema ni mara yake ya kwanza kutembelea Tanzania, hivyo atatumia nafasi hiyo ili kuweza kuutangaza utamaduni huo ipasavyo kwa kuangalia vivutio mbalimbali kupitia filamu hiyo kwa kutumia kipindi cha ‘Out of The World’.
Alisema kipindi chake huwa kinatazamwa na watu wapatao milioni 40 kutoka nchi mbalimbali.
Mpishi huyo anatarajiwa kuhudhuria hafla ya kuchangaisha fedha kwa ajili ya watoto wenye matatizo ya moyo leo jioni itakyofanyika kwenye hoteli hiyo.
|
No comments:
Post a Comment