Habari za Punde

*KAMATI YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI YATAKA RIPOTI ARV BANDIA KUTINGA BUNGENI

NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
 KAMATI ya Bunge inayoshughulikia masuala ya Ukimwi imeishauri serikali kutoa tamko la kuelezea ni hatua  gani inaendelea kuchukua baada ya kusimamisha kazi  baadhi ya viongozi wa Bohari Kuu ya Dawa   (MSD) kufuatia kuwepo kwa dawa bandia za kupunguza makali ya Ukimwi( ARV) katika kikao  cha Bunge kitakachoanza  mwishoni mwezi huu.
Kauli hiyo imetolewa leo na Mwenyekiti wa kamati hiyo, Lediana Mng’ong’o wakati akizungumza na waandishi wa habari kwenye ofisi ndogo za Bunge jijini Dares Salaam kuhusu kuwepo kwa dawa  hizo.
“ Sisi tungependa kuishauri  serikali kuendelea kufuatilia na hatua  za kisheria pale itakapobaini katika uchunguzi huo ili tatizo hili lisiendelee kutokea,” alisema Lediana ambaye ni Mbunge wa Viti Maalum Iringa.
Aliongeza kuwa  wanaishauri  Mamlaka cha Chakula na Dawa (TFDA) kuwa na wawakilishi katika kanda mbalimbali ili kuweza kudhibiti tatizo la kuwepo kwa dawa bandia.
Aidha kamati hiyo imelaani kampuni  ambayo imeingiza dawa feki na  imetaka hatua za kisheria zichukuliwe.
Kamati hiyo imewataka watu wanaotumia dawa hizo kutoziacha , bali waendelee kuzitumia kwa kuwa dawa  zote si feki na pia  zipo za kutosha.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.