Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia alipofungua Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hiz o. Mkutano huo umefunguliwa leo katika Ukumbi wa AICC, Jijini Arusha na kuhudhuriwa na mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kushoto) akipokea barua ya wazi kutoka kwa Katibu wa Mkuu wa Shirika la Utalii la Dunia, Taleb Rifai, iliyotolewa na Baraza la Waendesha Utalii Duniani (WTTC) mara baada ya kufungua Mkutano wa Kuhamasisha utalii barani Afrika leo, jijini Arusha. Katika Mkutano huo pia umehudhuriwa na Mawaziri 17 kutoka nchi mbalimbali za Afrika.
Baadhi ya Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wakifuatili kwa makini Hotuba ya makamu wa Rais, wakati wa ufunguzi huo.
Baadhi ya Mawaziri kutoka nchi mbalimbali wakifuatili kwa makini Hotuba ya makamu wa Rais, wakati wa ufunguzi huo.
Picha ya pamoja na baadhi ya viongozi.
Makamu akimfafanulia jambo mgeni wake, Katibu Mkuu wa Shirika la Utalii, Duniani, Taleb Rifai, kuhusu utamaduni wa kabila la wamasai.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akipunga mkono kuwaaga wasanii wa ngoma ya asili wa kabila la kimasai wakati akiondoka katika ukumbi wa mikutano wa AICC jijini Arusha leo, baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia Pakti ya kifuko cha unga wa Ubuyu na kusikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Masoko na Mauzo wa kampuni ya Moringa Consultancy (TZ) Co Ltd, Christina Ngoti, wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo jijini Arusha.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mtaalam wa Tiba za Asili, James Kangaa, wakati Makamu alipokuwa akitembelea Mabanda ya Maonyesho baada ya kufungua mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Kutangaza Utalii kwa Nchi za Bara la Afrika na Kuhamasisha Utalii Endelevu katika nchi hizo. Mkutano huo umefanyika leo, jijini Arusha.
No comments:
Post a Comment