Habari za Punde

*SABI ALIA KUCHEZEWA 'RAFU' UCHAGUZI WA UVCCM MKOA WA MARA

Aliyekuwa mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi (kulia) akifafanua jambo wakati alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na uchaguzi wa Umoja wa Vijana (UVCCM) mkoa wa Mara. Kushoto ni Sheweji Mkumbura, ambaye ni rafiki yake wa karibu. Picha na Mpiga Picha wetu
*******************************

Na Mwandishi wetu
ALIYEKUWA mgombea nafasi ya Uenyekiti wa Umoja wa Vijana Mkoa wa Mara, Gabriel Mnasa Sabi, ameuomba uongozi wa juu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) pamoja na Umoja wa Vijana makao makuu, kuingilia kati chaguzi za umoja wa vijana ambazo zimetawaliwa na vitendo vya hujuma na rushwa.
 
Sabi ambaye juzi aishindwa kwa tofauti ya kura 14 dhidi ya Ditu Manko , alisema kuwa uchaguzi wao haukuwa huru na haki kwani matokeo yalijulikana kabla ya kupiga kura.

Aidha Sabi, alisema kuwa alitangaziwa matokeo hayo wakati wa kampeni kwa madai kuwa nafasi ya uenyekiti lazima itoke wilaya ya Tarime kutokana na nguvu ya kifedha.

“Hali hiyo ilinifanya kunyong’onyea hata kabla ya uchaguzi, hata hivyo nilipiga moyo konde na kuingia kwenye uchaguzi, matokeo yakawa yaleyale, nilishangazwa sana na wafuasi wangu wakaamua kutoendelea na uchaguzi huo,” alisema Sabi.
 
Alisema kuwa baada ya matokeo hayo, fujo zikaanza kwani wafuasi wake walichoka kuona vitendo vya uonevu vya waziwazi na kuongeza kuwa pamoja na wafuasi wake kutoka, uchaguzi huo uliendelea na kuhoji hao waliochaguliwa walipata kura hizo kutoka wapi, ''kwani sidhani kama idadi ya wapiga kura kwa mujibu wa katiba ilifikiwa''.
 
“Kasoro hizi si za kuziacha kwani zinawagawa wanachama, ni lazima zikemewe  kwani bado kuna chaguzi nyingi ndani ya chama,” alisema.

Alifafanua kwa kusema kuwa hana tatizo na uongozi wa juu wa CCM kutokana na sera madhubuti zenye kuleta maendeleo ya nchi, ila kilio chake ni viongozi wanaokipaka matope chama hasa wa ngazi ya chini.


No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.