Na Mwandishi Wetu
BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini Thomas Mashali amesaini mkataba wa kucheza pambano la ubingwa wa Afrika Mashariki na Kati dhidi ya Bondia Medi Sebyala wa Uganda, litakalofanyika Oktoba 14 mwaka huu kwenye Ukumbi wa Friends Corner, jijini Dar es Salaam.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, hivi karibuni, Mratibu wa Pambano hilo linalosimamiwa na Shirikisho la Ngumi za kulipwa TPBO, Regina Gwae, amesema mpambano huo ni maandalizi ya kuhakikisha bondia Mashali anavuka mipaka ya Tanzania baada ya kufanya vema nchini.
“Huwezi kwenda nje kama ndani hufanyi vizuri na huwezi kwenda Ulaya, ukaikimbia Afrika Mashariki, hivyo tumeona tumpe pambano Afrika Mashariki ili akifanya vyema aweze kuvuka mipaka hiyo sasa,” alisema Regina.
Aliongeza kuwa, mazungumzo na bondia Sebyala yamekamilika na tayari ameshatumiwa mkataba wake kwa ajili ya pambano hilo ili ausaini baada ya kuupitia.
“Pambano hilo litakuwa na raundi 10 na watacheza katika uzito wa kilo 72 na kama tujuavyo ukizungumzia mabondia wa uzito wa kati wanaotamba nchini na Afrika Mashariki kwa ujumla, huwezi kuacha kuwataja Mashali na Sebyala,” alisema Regina.
Regina alisema wanataraji mpambano utakuwa mzuri wenye kuvutia kwa kuwa Mashali ni bondia mzuri na Sebyala naye ni mzuri aliyeweka historia ya kuwasumbua mabondia mahiri nchini Fransis Cheka na Rashidi Matumla kwa nyakati Tofauti.
Pia amewaomba wafadhili kujitokeza kudhamini mchezo huo unaotarajiwa kuwa na mapambano kadhaa ya utangulizi yenye kuvutia wakiwemo mabondia chipkizi Ibrahimu Class 'King Class Mawe' na Jonas Segu, mabondia wengine watakacheza utangulizi watatangazwa baadaye watakaosindikiza mpambano huo.
Katika Mchezo huo kutakua na Uhuzwaji wa DVD za mafunzo ya mchezo wa ngumi pamoja na kutambua sheria zake mbalimbali zitakazokua zikisambazwa na kocha wa mchezo huo mkoa wa kimichezo wa Ilala Rajabu Mhamila 'Super D' kwa ajili ya kuwapa mambondia mbalimbali mbinu za mchezo na mashabiki kujua sheria za masumbwi.
Ndani yake wakiwemo mabondia Floyd Mywether, Manny Paquaio, Amiri Khani, Mohamedi Ali, Mike Tayson David Haye na wengine ambapo kutakuwa na matukio ya mazoezi yao katika mataifa yao ikumbukwe kuwa ni mabingwa wa dunia. na kutakuwa na mapambano makubwa matano ya utangulizi.
No comments:
Post a Comment