Habari za Punde

*UZINDUZI WA TAARIFA YA AWALI YA MAGONJWA YA UKIMWI NA MARALIA

Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akizindua matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya magonjwa ya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012 uliofanyika leo katika hoteli ya ya Blue Pearl Ubungo plaza  jijini Dar es Salaam huku Mkurugenzi Mkuu wa NBS Dkt. Albina Chuwa akimuangalia kwa makini. Utafiti huo utatoa viwango vya sasa vya maambukizi ya magonjwa hayo katika kuelezea hali halisi ya sasa ya viashiria ilivyo katika mpango wa MKUKUTA na MKUZA katika Malengo ya Milenia ya 2015. 
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akimkabidhi Dkt. Jesicca Kafuko kutoka USAID  kitabu chenye matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya magonjwa ya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012 ili wakaifanyie kazi . Uzinduzi wa huo  uliofanyika leo katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo plaza  jijini Dar es Salaam.
 Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akimkabidhi  Khazija Khamis mwakilishi kutoka  wizara ya Afya Zanzibar  matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012 ili wizara hiyo ikaifanyie kazi. Uzinduzi wa ripoti hiyo uliofanyika leo katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo plaza  jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Hussein Mwinyi akiwaonyesha wadau mbalimbali waliohudhuria uzinduzi wa   taarifa ya matokeo ya awali yanayohusiana na ugonjwa wa Malaria kutoka katika Utafiti wa viashiria vya  magonjwa ya Ukimwi na Malaria wa mwaka 2011 – 2012. Hafla hiyo ilifanyika  leo katika hoteli ya Blue Pearl Ubungo plaza  jijini Dar es Salaam.Picha na Anna Nkinda – Maelezo

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.