Habari za Punde

*WANNE WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI (W) BAHI-DODOMA

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen. 

Na. Luppy Kung’alo wa Jeshi la Polisi Dodoma
Abiria wanne waliokuwa wakisafiri katika Daladala (Hiace) iliyokuwa inatokea Dodoma kuelekea kijiji cha Mkanda wilayani Manyoni Mkoa Singida wamepoteza Maisha katika tukio la ajali na kuwaacha abiria wengine kumi na nane wakiwa majeruhi.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma Bw. Zelothe Stephen alithibitisha kutokea kwa ajali hiyo akieleza kuwa ilitokea siku ya Jumapili tarehe 14/10/2012 majira ya  saa kumi jioni (16:00hrs) katika Kijiji cha Uhelela Kata ya Bahi Wilaya ya Bahi Mkoa wa Dodoma katika  barabara kuu ya Dodoma/Singida.

Bw. Zelothe Stephen alisema  ajali hiyo ilihusisha gari lenye namba za usajili T.518 AVQ aina ya SCANIA likiwa na  tela lenye namba za usajili T.780 AVK lililokuwa linaendeshwa na Dereva TUTU  ACKSON mwenye umri wa miaka 23, Mkazi wa Chaduru, na gari namba T. 803 AHX aina ya TOYOTA HIACE lililokuwa likiendeshwa na DANIEL  JACKSON mwenye umri wa miaka 46, mkazi wa Dodoma.

Aliwataja waliopoteza Maisha katika ajali hiyo kuwa ni abiria wanne waliokuwa wakisafiri na Hiace hiyo ambao ni MASHAKA ELIA mwenye umri wa miaka (27) ambaye ni  kondakta, mkazi wa Chang’ombe Mkoani Dodoma, MOSI MAUNDAA mwenye umri wa miaka (55) mkazi wa wilaya ya manyoni, EZEKIELI MASALITO mwenye umri wa miaka kati ya (40-45) mkazi wa Makanda wilaya ya Manyoni na DASTAN KIPINGU mwenye umri wa miaka (35) ambaye hakufahamika ni mkazi wa wapi.

Mkuu huyo wa Polisi Mkoa wa Dododma alisema Miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Kituo cha Afya cha Wilaya ya Bahi ikisubiri kuletwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa Uchunguzi zaidi wa Daktari, wakati majeruhi wengine kumi na tano (15) wamelazwa katika Hospitali ya Mkoa wa Dodoma kwa matibabu zaidi.

“Katika ajali hiyo Abiria kumi na nane (18) walijeruhiwa  akiwemo Dereva wa Daladala hiyo, ambapo kati yao wanaume waliojeruhiwa ni 15 akiwemo mtoto mdogo mmoja na wanawake watatu (3).” Alifafanua Kamanda Zelothe

Bw. Zelothe aliwataja  waliotibiwa na kuruhusiwa kuwa ni ESTER FUNGA mwenye umri wa miaka (30) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, aliyejeruhiwa katika mkono wa kushoto na  usoni, CHRISTINA DANIEL mwenye umri wa miaka (25) mhudumu wa hoteli,  mkazi wa Ipagala, ambaye ameumia mkono wa kulia na mguu wa kulia  na GREYSON  OMARY mwenye umri wa mwaka mmoja na nusu, mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni ambaye ameumia kichwani.

 Aidha Kamanda Zelothe alitaja orodha ya majina ya waliojeruhiwa kuwa ni
DANIEL  JACKSON @ NZOYA mwenye umri wa miaka (46) Dereva wa Toyota Hiace, mkazi wa Bahi road Dodoma, ANTONY  CHAKA mwenye umri wa miaka (23) mkazi wa Makanda Manyoni, JOSEPH  CHRISOPHER mwenye umri wa miaka (40)  mkazi wa Makanda, VENANCE  MIRAJI mwenye umri wa miaka (40)  mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, MASONGA  BURUGE mwenye umri wa miaka (40)  mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, PROTAS  MWALUKO mwenye umri wa miaka (70) mkazi wa Makanda wilayani Manyoni na PEASON  MAGUMILA mwenye umri wa miaka (30)  mkazi wa Kibaigwa wilayani Kongwa.

Wengine ni TIMITA  MADATILO mwenye umri wa miaka (30)  mkazi wa Makanda wilayani Manyoni, MATONYA  MWENDAUHEMBA mwenye umri wa miaka (40) mkazi wa wilaya ya Bahi, MASHAKA  ELIA mwenye umri wa miaka (27)  mkazi wa Chang’ombe Dodoma, TITUS  MTWEVE mwenye umri wa miaka (32) mwalimu wa shule ya sekondari Manyoni, JUMA SHABANI mwenye umri wa miaka (35) mkazi wa Makanda wilyani Manyoni, SOPHIA  LEMA mwenye umri wa miaka (52) mkazi wa Kintinku wilayani Manyoni, RAMADHANI ABDALLAH mwenye umri wa miaka (38)  mkazi wa wilyani Manyoni na mwanaume ambaye hajafahamika jina mwenye umri kati ya (35-40) ambaye hali yake ni mbaya.

Bw. Zelothe Stephen alisema uchunguzi wa awali unaonyesha kuwa chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa dereva wa lori hilo ambaye aliigonga kwa nyuma gari hilo la abiria iliyokuwa mbele yake na kuitoa  nje ya barabara na kusababisha ajali hiyo, Dereva wa Lori hilo lililokuwa linatoka Dar es Salaam likielekea Kigoma  amekamatwa na utaratibu wa kumfikisha mahakamani unaandaliwa.

Imetolewa na
POLISI MKOA WA DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA MAHUSIANO,
 CONTACT:
Phone:  0715 006523, Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone:  0712  360203, Silyvester Onesmo – Police  Konstebo  (PC)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.