Habari za Punde

*WAREMBO WA REDD'S MISS TANZANIA 2012 WAANZA KUPANDA MLIMA KILIMANJARO

Warembo wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2012, wakiwa katika picha ya pamoja, jana wakati warembo hao walipo tembelea Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro na kuopata maelezo na kuzungumza na watalii na wapanda mlima huo. 
Warembo 29 na viongozi wa  Kamati ya Miss Tanzania wapo Kanda ya Kaskazini kutembelea vivutio vya utalii na kuhamasisha utalii wa ndani.

Mbali na kutembelea hifadhi hiyo lakini warembo hao walishiriki katika tamasha la michezo kwa ajili ya kuchangia fedha na vitu mbalimbali vya watoto Yatima vya jijini Arusha.

Leo Oktoba 8 warembo wanaendelea na ziara yao ikiwa ni pamoja na kutembelea kituo cha Redio cha RADIO 5 cha jijini Arusha.
 Washiriki wa Redds Miss tanzania 2012 wakiwa katiak picha tofauti tofauti wakati wakiwa katika eneo la Hifadhi ya Mlima Kilimanjaro KINAPA.
  Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanao panda mlima Kilimanjaro.
 Baadhi ya warembo wakipiga picha na baadhi ya viongozi wa Kamati ya Miss Tanzania
  Warembo wakizungumza na mmoja wa Wasaidizi wa watalii wanaopanda mlima Kilimanjaro.
 Warembo wakiwa wakiwa katika eneo la maegesho ya magari KINAPA
 Wakielekea eneo la kupata taarifa mbalimbali za Mlima Kilimanajaro
 Wakipiga picha na baadhi ya watalii waliowakuta hapo.
 Warembo wa Redds Miss Tanzania wakimsikiliza Ofisa Mhifadhi wa KINAPA, Eva Malya, aliyekuwa akiwapa taarifa mbalimbali juu ya mlima huo.
 Warembo wakiwa na nyuso za furaha wakiendelea kupata maelekezo kuhusu taratibu za kupanda mlima.
Hapa sasa walibeba mabegi ili kuanza kupanda Mlima.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.