Meneja
mradi wa shirika lisilo la kiserikali linalowajengea uwezo wajasiriamali kwa
kutumia teknolojia ya habari na mawasiliano katika kupambana na umaskini( EIFL)
Monica Elbert (mzungu) akipokea maelezo kwa mjasirimali Geofrey Nkong’o (wa pili
kushoto) huko Kitunda -DSM kuhusu watakavyonufaika na
mafunzo waliyoyapata kupitia mpango wa
kufundishia wa teknolojia ya habari na mawasiliano ujulikanao (Public Library
Innovation Programme- PIP) ambapo, shirika hili linafadhili Maktaba ya Taifa
nchini (TLSB) ili ziweze kutumia teknolojia hiyo katika kuwaletea mawasiliano wajasirimali katika kupata habari kwa ajili ya matumizi mbalimbali katika
shughuli zao za kila siku na maendeleo.
Meneja
mradi wa shirika la (EIFL) Monica Elbert kutoka Ujerumani (kulia) akimsikiliza Katibu wa kikundi cha wajasiriamali
wa Kiyombo Kitunda mkoani Dar es Salaam Yesaya Mbwambo, (katikati) wakati
wakiangalia baadhi ya mabanda ya ufugaji wa kuku na jinsi wajasiriamali watakavyonufaika baada ya kumaliza mafunzo ya teknolojia ya
habari na mawasliliano, ambapo wataweza
kutafuta taarifa mbalimbali kupitia mtandao na zikiwepo za utafutaji wa masoko
pamoja na shughuli zao za kila siku, (kushoto) ni Mwenyekiti wa kikundi
cha (KUK) Wambura Mugasa.
Meneja
mradi washirika lisilo la kiserikali kutoka Ujerumani (EIFL) Bibi Monica Elbert
(kulia) akiwashukuru wanakikundi wajasiriamali cha ufugaji kuku wa Kiyombo
Kitunda (KUK) baada ya kumpatia zawadi ya
vazi la kitenge kwaajili ya kumbukumbu, baada ya kuwatembelea mishoni
mwa wiki na kuangalia shughuli zao za ufugaji. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
No comments:
Post a Comment