Habari za Punde

*ABIRIA WA TRENI YA MWAKYEMBE KAMA WA MBAGALA, WAGEUZA NALO KUWAHI SITI

 Baadhi ya Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa wanasubiri treni ya mwakyembe iwasili stesheni ikitokea ubungo maziwa tayari kwa safari ya kuwarudisha Majumbani Kwao. 
 
Abiria wakianza kupanda treni tayari kwa kurejea makwao mara baada ya treni la mwakyembe kuwasili kituoni hapo kwenye majira ya saa kumi na moja na dakika ishirini jana.
 Mmoja wa Abiria aliyegeuza na treni hilo aliyepandia Kituo cha Kamata, kwa lengo la kuwahi kiti akibishana na mmoja wa abiria aliyechini katika foleni.
Wakazi wa Jiji la Dar wakiwa kwenye foleni ya kupanda treni maarufu kwa jina la treni ya mwakyembe jana kwenye majira ya saa 11 jioni katika kituo cha Stesheni.
Wakazi wa jiji la Dar wakipanda kwenye treni la mwakyembe mara baada ya kuwasili kwenye kituo chake cha Stesheni jana Kwenye majira ya Saa 11 Jioni, tayari kwa kuwarudisha majumbani kwao likitokea Mjini kuelekea Ubungo ambapo ndio kituo cha Mwisho.
**************************
ABIRIA wanaotumia usafiri wa Treni, nao wameiga staili ya abiria wa Mbagala, ambapo hulazimika kila jioni na asubuhi abiria katika kituo cha Treni cha Stesheni kupanda Treni hilo na kugeuza nalo, jambo ambalo huwafanya abiria wanaosubiria usafiri huo mwisho wa kituo kukosa nafasi na siti kutoka na treni hilo kufika kituoni likiwa tayari limejaa.

Abiria waliokuwa wakisubiria treni hilo walianza kulalamika baada ya kuona kila behewa likiwa tayari limeshajaa kabla hata treni hiyo haijafika kwenye kituo chake cha mwisho kwa lengo la abiria hao kuwahi . 

Baada ya Tukio hilo kutokea kulizuka sintofahamu kwa baadhi ya wafanyakazi na Askari Polisi ambao hawajawahi kuona utaratibu huo ukifanyika na kupelekea Abiria kuhisi tayari wafanyakazi wa treni hiyo waneshaanza kuchakachua kitu ambacho utaratibu hauruhusu. 

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.