Habari za Punde

*FM ACADEMIA KUADHIMISHA MIAKA 15 DESEMBA 14 KWA KUANGUSHA BONGE LA SHOO


BENDI ya Fm Academia imeandaa Party maalum ya kuadhimisha miaka 15 tangu kuanzishwa kwa bendi hiyo ya  muziki wa dansi, nchini.

Sherehe hiyo ya Fm Academia ‘Wazee wa Ngwasuma’ inatarajia kufanyika Desemba 14 kwenye ukumbi wa Msasani Club.
 
Akizungumza na Mtandano huu wa www.sufianimafoto.blogspot.com, Mratibu wa onyesho hilo maalum, Nassib Mahinya, alisema kuwa, usiku huo wa aina yake utaambatana na shamrashamra mbalimbali zilizoandaliwa ili kuwapa raha mashabiki wa bendi hiyo na mashabiki wa muziki wa dansi kwa ujumla wawatakaohudhuria onyesho hilo.

Aidha Nassib, alisema kuwa kupitia usiku huo utakuwa ni maalum utakaowakutanisha wanamuziki mbalimbali waliowahi kupitia katika bendi hiyo kabla ya kuhama na wengine kuanzisha bendi zao tangu bendi hiyo ilipouwa ikianzishwa rasmi kama Kina Ndanda Kossovo na Maluu Stonc, Saji Mwila, Pacheko Mbongo, Totoo Ze bingwa na wengine wengi.

Pia bendi hiyo itapiga  nyimbo zake zote kuanzia zile zilizopata kutamba siku za nyumba tangu kuanzishwa kwake kama Jela, Jimmy Chocolate na nyinginezo, kuanzia albama ya kwanza ya bendi hiyo hadi nyimbo mpya za sasa.

“Lakini pia kutakuwa na tukio la kukata keki sambamba na kuwapongeza wale wote waliochangia kwa namna moja ama nyingine kuifikisha bendi yetu mahala ilipo kwa sasa”. alisema, Nassib
 
Nassib, aliongeza kuwa katika kunogesha zaidi usiku huo wanatarajia kualika makundi mbalimbali ya burudani ili kusindikiza maadhimisho hayo, ambapo tayari baadhi kama kundi la Mapacha watatu pamoja na wasanii wa kundi la Mtanashati Entertauinment wakiwemo Dogo Janja, PNC na wengineo, wamekwisha thibitisha kushiriki.
 
Onyesho hilo limeandaliwa na Sinai Entertainment na kudhaminiwa na Mabibo Beer Wine & Spirit, Mama Mbaga Catering, Africa Media Group, Chonapi General Supplier, Benny Mlokozi Company , Big Solution, Mtanashati Entertainment, Eliado Point View, Arafa Salon, Friendship Restaurant, Masters Club.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.