Habari za Punde

*JK AACHIA NGAZI UENYEKITI WA CCM, WAJUMBE KUANZA KUMPIGIA KURA MUDA SI MREFU

 Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete na Makamu wake wa Uenyekiti Dk. Amani Abeid Karume (Zanzibar) na Pius Msekwa (Bara) wakiondoka meza kuubaada ya kujiuzulu nafasi zao kufuatia kumaliza muda wao wa uongozi. Baadaye Kikwete ambaye ameteuliwa na CCM kugombea tena nafasi hiyo ya Uenyekiti alikaa upande wa wajumbe kushubiri kuchaguliwa tena. Tukio hili limefanyika saa 9:15 alasiri.
 Kikwete na meza kuu wakiwa upande wa wajumbe wa Mkutano Mkuu, wakati uchaguzi Mkuu kumpata Mwenyekiti mpya wa CCM Taifa ambapo yeye ni mgombea pekee.
Mwenyekiti Mstaafu wa CCM, Benjamin Mkapa akiongoza Mkutano Mkuu kwa muda baada ya Kikwete kujiuzulu. Sasa mchakato wa upigaji kura kuchagua Mwenyekiti na kuwapata Makamu Wenyeviti Bara na Zanzibar unaendelea muda huu. FUatilia hapa kupata matokeo (Picha zote na Bashir Nkoromo)

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.