Mkazi wa Kijiji kimoja kilichomo katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera, akisafirisha Nyama ya Wanyama Pori, ambayo haikuweza kufahamika kwa hara ni nyama ya mnyama gani, ambapo muda mchache kabla ya jamaa huyu eneo hili walipita wengine wawili wakiwa wameongozana huku pia wakiwa wamebeba nyama kama hii, ambayo imeelezwa hupelekwa kuuzwa kijiji cha mbele ambako kumechangamka kutokana na mabasi mengi kusimama maeneo hayo ambayo jamaa hawa hufanya biashara ya kuchoma nyama hii.
Hivyo wasafiri kueni makini kula hovyo nyama za kuchoma njiani msizozijua kwa haraka kwani unaweza kula usichokitarajia na pia usafirishaji huu na uwindaji haramu kama huu huendelea katika maeneo kama haya kutokana na wasimamizi wa sheria zilizowekwa kuwa wakifanyika kazi zao mojini tu bila kufika katika maeneo husika.
No comments:
Post a Comment