Habari za Punde

*SIMBA 0 TOTO 1 TAIFA, AZAM CHALI 2-1 KWA MGAMBO

Timu ya Simba ya jijini Dar es Salaam, leo jioni imepokea kichapo cha bao 1-0 kutoka kwa Toto Africa ya jijini Mwanza, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini. Bao la Toto Africa limefungwa Dakika ya 73 na Mussa Said Kimbu, kwa kichwa kufuatia mpira wa adhabu ndogo, uliopigwa na Mohamed Jingo. 

WAKATI Huo huo, Timu ya Azam Fc ya jijini Dar es Salaam, nayo imekubali kipigo cha mabao 2-1, dhidi ya JKT Mgambo ya Tanga, katika mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Mkwakwani, jijini Tanga. Mabao ya Mgambo yamefungwa na Issa Kindulu, huku bao la kufutia machozi la Azam, likiwekwa kimiani na Kipre Tchetche.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.