Zungu |
NA MWANDISHI WETU, DODOMA
WATU watano akiwemo mbunge wa Ilala Musa Zungu wamekamatwa na Taasisi ya
kuzuia na Kupambana na Rushwa Mkoani Dodoma wakidaiwa kutoa rushwa kwa
wajumbe wa Jumuiya ya Wazazi ili wawachague.
Kamanda wa Taasisi hiyo Eunice Mmari alisema Zungu alikamatwa katika
Hotel ya Golden Crown jana kati ya saa mbili na nusu na saa tatu usiku.
Eunice alisema baa ya taasisi yake kupata taarifa hizo walianza
kumfatilia kwa karibu mgombea huyo na ndipo walipomsikia akitoa maagizo
kupitia simu ya mkononi kuagia nani apewe kiasi gani.
Alisema baada ya hatua hiyo TAKUKURU walianza kumfatilia Zungu na ndipo
waligundua kuwa yupo katika gari ndogo aina ya Toyota Mark –II huku
akifuatana na gari jingine aina ya Prado ambalo ndiko fedha na wapambe
wake walikuwa wamepanda.
Alisema baa da kulisimamisha gari hilo alilokuwemo Zungu ghafla Prado
hilo liliweza kutoroka na kumuacha Zungu na ndipo alipokamtwa na
kuhojiwa.
Alisema hata hivyo TAKUKURU waliweza kufuatilia mitandao ya simu na
kisha kubaini kuwa fedha hizo zilikuwa zikigawiwa na mmoja wa wakala
wake ambaye naye kwa sasa wamekamtwa.
Kamanda huyo aliwataja wengine waliokamatwa na Zungu ni pamoja na
Yahya Khamis Danga , Busulo Mohamed Pazi na Famik Joseph Mang’ati.
Alisema kwa sasa watuhumiwa hao wote wameachiwa kwa dhamana huku
uchunguzi zaidi ukiendelea na watafikishwa mara baada ya kukamilika.
Aidha kamanda huyo alisema mwingine aliyekamtwa ni pamoja na Fatuma
Kasenga ambaye ni mwenyekiti wa jumuiya ya Wazazi kutoka Mkoa wa Mbeya.
Alisema mwenyekiti huyo alikamatwa usiku wa kuamkia leo, saa tisa usiku
katika hoteli ya Kitoli mjini hapa akiwanunulia wajumbe wake chakula.
Kamanda huyo apia alisema kuna taarifa zaidi ambazo zinamtaja Alhaji
Abdalah Bulembo kuwa naye amekuwa akitajwa sana katika utoaji huo wa
rushwa.
Alisema hata hivyo wanaendelea na uchunguzi dhidi ya tuhuma za Bulembo
na wamepata taarifa za awali kuwa anatoa rushwa hizo nyumbani.
No comments:
Post a Comment