Mkurugenzi wa Takwimu nchini, Morrice Oyuke, akisoma hotuba yake kumwakilisha Mkurugenzi Mkuu wa TAKWIMU nchini Dkt.. Albina Chuwa, wakati wa kongamano la pili la mwaka la wadau wa TAKWIMU nchini lililofanyika leo jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka Benki ya Dunia, Thomas Danielewitz, akitoa hotuba yake leo jijini Dar es Salaam katika ufunguzi wa kongamano la pili la mwaka kwa Wadau wa Takwimu nchini. Kongamano hilo la siku moja limefunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha Dkt. Saada M. Salum (hayupo Pichani).
Baadhi ya washiriki wa kongamano la pili la mwaka unaowashirikisha Wadau wa Takwimu nchini wakimsikilza Naibu Waziri wa Fedha Dr. Saada M. Salum (hayupo pichani) katika ufunguzi wa kongamano hilo leo jijini Dar es Salaam.
Naibu wa Wizara ya Fedha Dkt. Saada M. Salum akifungua kongamano la pili la mwaka kwa wadau wa Takwimu nchini leo jijini Dar es Salaam., ambapo amewasisitiza wadau kutumia takwimu zilizo sahihi. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
No comments:
Post a Comment