Watanzania waishio Ujerumani kufanya hafla ya kumuaga Mhe,Balozi Bw.Ahmada Ngemera ! Jumamosi 08-December 2012 mjini Berlin,Ujerumani.
Umoja wa Tanzania Ujerumani (UTU) unaheshima kubwa kutarifu na kuwaomba watanzania wote wanaoishi ujerumani na jirani ya Ujerumani kuwa umoja wetu tunatarajia kufanya afla ya kumuaga Mheshimiwa balozi, Ahmada Ngemera, ambaye anamaliza muda wake wa kufanya kazi.
Mhe. Balozi bwana Ahmada Ngemera amekua balozi wa Tanzania nchini Ujerumani na watanzania wanaoishi ujerumani watamkumbuka daima Mheshimiwa Balozi Bw.Ahmada Ngemera kwa kuwa karibu sana na jamii ya watanzania,pia atakumbukwa kwa jitihada zake au kile ambacho watanzania
wa ujerumani wanachokiita kuasisi Umoja na mshikamano wa watanzania nchi ujerumani,ambapo Mhe. Balozi, Ngemera na msaidizi wake Mhe.Bw.Ali Siwa wahamua kuhamasisha watanzania waishio Ujerumani kuungana katika kila hali kuanzisha umoja wa mshikamano wa watanzania,kitu
ambacho mabalozi wengi walishindwa kufanikiwa kufanya labda kwa sababu ya ukubwa wa nchi ya ujerumani wa watanzania wanaishi katika miji mbali mbali,lakini kazi hiyo ya kuwaungunganisha watanzania, Balozi Bw.Ahmada Ngemera na Msaidizi wake Bw.Ali Siwa walifanikiwa kuwafikia watanzania wote waishio Ujerumani na kuwashauri waanzishe umoja wa mshikimano,na matunda ya juhudi zao ndipo kukazaliwa Umoja wa waTanzania Ujerumani.(UTU) Umoja ambao ni chombo cha watanzania wote ! chombo ambacho watanzania waishio ujerumani wanajivunia .
UMOJA NA MSHIKAMANO NDIO MSINGI WETU IMARA!
OMBI:
TUNAWAOMBA WATANZANIA WOTE ! NA MARAFIKI WOTE WA TANZANIA
AMBAO WANATAKA KUSHIRIKI KATIKA AFLA HII,
TUNAOMBA MTOE MCHANGO WA EURO 20.00 NA KWA WANAFUNZI EURO 10.00 TU
kwa kupitia Account : Union of Tanzania in German e.V.
VR Bank Rosenheim-Chiemsee AG
Konto-No.: 59641 BLZ: 71160161
Verwendungszweck: „Kumuaga Mhe. Balozi Ngemera
Pia unaweza kuwasiliana na kamati.utu@googlemail.com
No comments:
Post a Comment