Mchezo wa Kirafiki wa Kimataifa kati ya timu ya Tanzania Taifa Stars na Zambia 'Chipolopolo' umemalizika hivi punde, huku Stars wakiibuka na ushindi wa bao 1-0, Bao lililofungwa na Mrisho Ngassa, katika Dakika ya 45 ya kipindi cha kwanza bao lililodumu hadi kumalizika kwa mchezo huo, uliochezwa katika Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.
Kipindi cha pili Kocha Mkuu Kim, alifanya mabadiliko kwa kumtoa Mrisho Ngassa, ambapo nafasi yake ilichukuliwa na Amir Maftah, na Kelvin Yondani, aliyeumia na nafasi yake ikachukuliwa na Naadir Haroub 'Canavaro' na Simon Msuva, mbaye aliingia kuchukua nafasi ya Hamis Mcha, aliyeumia, mabadiloko yaliyozidi kuimarisha safu ya ulinzi.
No comments:
Post a Comment