Makocha wa Tanzania (Taifa Stars), Kim Poulsen na Zambia
(Chipolopolo) watakuwa na mkutano na waandishi wa habari utakaofanyika kesho
(Desemba 21 mwaka huu) kuzungumzia pambano lao litakalochezwa Jumamosi (Desemba
22 mwaka huu) Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Mkutano huo utafanyika saa 5 asubuhi kwenye ukumbi wa
mikutano wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF). Makocha hao
watazungumzia maandalizi yao ya mwisho kabla ya pambano hilo litakalochezeshwa
na mwamuzi Sylvester Kirwa kuanzia saa 10 kamili jioni.
Pia makocha hao watajibu maswali kutoka kwa waandishi wa
habari kuhusu pambano hilo litakalokutanisha timu hizo ambazo zimefanya vizuri
kwenye orodha ya viwango vya ubora vya Shirikisho la Kimataifa la Mpira wa Miguu
(FIFA) vilivyotolewa jana (Desemba 19 mwaka huu).
Wakati Zambia ambao ni mabingwa wa Afrika wamepanda juu
kwa viwango vya ubora kwa nafasi nne, Taifa Stars ambayo katika mchezo uliopita
iliifunga Kenya (Harambee Stars) bao 1-0 imepanda kwa nafasi nne.
Taifa Stars ambayo inadhaminiwa na Kilimanjaro Premium
Lager iko kambini tangu Desemba 12 mwaka huu kujiandaa kwa mechi hiyo kubwa ya
kirafiki inayotarajiwa kuwa ya kuvutia.
No comments:
Post a Comment