Wafuasi wa Lema wakishangilia barabarani wakati Mbunge huyo akipita.
Mbwembwe za waendesha pikipiki wengine ziliwashinda na kupata aibu kama hii kwa sifa za kijinga.
Furaha hiyo ilikuwa kwa kila aliye Mwanachadema.
Skafu na vitu mbalimbali vilivyo na alama ya Chadema viliuzwa jijini Arusha kwa wingi.
Mke wa Mbunge Godbless Lema akiwa kwenye gari pamoja na mtoto wao wakati wa mapokezi hayo.
Lema Arusha anafananishwa na Barack Obama.
Watu walining'inia katika magari bila hofu.
Huyu 'eti' alikua anachukua kumbukumbu za Video kwa mbwembwe na lenzi zisizo na kamera.
Lema akiwa na Mbunge wa Arumeru Mashuari CHADEMA, Joshua Nasari.
WAFUASI wa Chadema leo wamempokea Mbunge wao kupitia tiketi ya CHADEMA, Godbless Lema kwa shambra shambra na bashasha katika jiji la Arusha, ambapo msafara umeanzia Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) hadi katika Viwanja vya Kilombero, alipohutumia maelfu ya wana CHADEMA wa Arusha Mjini.
Mapokezi hayo yamefanyika wakati Godbless Lema alipokuwa akirejea mjini Arusha akitokea jijini Dar es Salaam kusikiliza hukumu ya Rufani ya Keshi yake ya Kuvuliwa Ubunge iliyotolewa maamuzi ya kumrejeshea Ubunge wake Desemba 21,2012.
Maelfu ya wananchi wakiwa katika msafara mrefu zaidi ya pikipiki 500 na magari ulianzia Uwanja wa Ndege KIA mara baada ya Mbunge huyo kuwasili uwanjanai hapo majira ya saa 4:20 Asubuhi
No comments:
Post a Comment