Imepita muda sasa toka lilipotoka tangazo la kuwazuia watu wanaowatumia wanyama kama usafiri wa kubebea mizigizo kuacha kufanya hivyo, lakini cha kushangaza hadi sasa zoezi hilo halijafanyiwa kazi na wahusika kiasi cha kuwafanya watu kuwatumia wanyama kama usafiri wao wa kawaida kama anavyoonekana jamaa huyu pichani, (kushoto kwake) ni mwendesha Pikipiki na kulia kwake ni mwendesha Baiskeli, wakiwa sambamba katika Barabara ya Mwanakwerekwe, jana. Wengine utwakuta wakipakia mzigo mzito ambao hata Pick up haiwezi kubeba lakini wao huwapakia wanyama hawa na kisha kuwacharaza bakora ili waweze kutembea kwa mwendo kasi waweze kuwahi kwenda na kurudia mzigo mwingine, jambo ambalo halifai kwa Haki za binadam na wanyama pia.
Huyu naye katika Pikipiki Namba Z 893 DB akiwa kampakata mbuzi huku wakiwa katika mwendo.
Na je upakiaji wa mizigo na abiria kama hivi katika Chai Maharage hizi utakwisha zama gani??
Gari la abiria likiwa limepakia abiria na mzigo mkubwa juu, huku likikatiza mbele ya macha ya askari wa usalama barabarani bila kuonywa wala kukamatwa, sasa hali hii itakwisha mjini Zanziba kweli??
No comments:
Post a Comment