Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma, D. A. MISIME – ACP.
JESHI la Polisi Mkoa wa Dodoma,
linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za kujihusisha na shughuli za wizi wa
mtandao hususani katika maduka yanayotoa huduma za M-PESA,Tigo Pesa na Airtel
Money katika maeneo mbalimbali ya Manispaa ya Dodoma.
Watu hao ambao wanadaiwa kujipatia
zaidi ya shilingi 1,730,000 /= kwa Mawakala wanne tofauti wanaotoa huduma hizo
walikamatwa jana tarehe 19/12/2012 majira ya saa 12:00 hrs mchana.
Watuhumiwa hao ambao wanatokea Jijini
Dar es Salaam majina yao ni Mohamed s/o Dotto @ Sefu, mwenye umri wa miaka (30)
Mnyamwezi mkazi wa Kigogo, Mohamed s/o Pazi, Mzaramo Miaka (28)
na Ally s/o Mohamed miaka (25) ambao ni wakazi wa
Ilala.
Wamekuwa wakitumia mbinu mbalimbali
kufanikisha wizi huo, moja ya mbinu ni kwenda kwenye maduka yanayotoa huduma
hizo na kumwambia wakala kuwa wanaharaka na kutaka kuweka Pesa
kiasi fulani ambacho wanakuwa nazo mkononi na kuanza
kuzihesabu.
Mara meseji ya pesa toka kwa wakala
zinapoingia katika simu zao, simu zao huita wakati huo huo na
kujifanya wanapokea simu huku wakisogea pembeni
wakiongea na simu na kuondoka julma kwenda kuzitoa mahala pengine kwa
haraka.
Wakala walioathirika na Wezi hao
mpaka sasa ni Consolata d/o Martini ambaye duka lake liko eneo la Kuu Streetu
shilingi 300,000/=, Perndo d/o Martin qambaye Duka lake liko eneo la CBE Tsh.
860,000/= Mlay s/o Felix eneo la Makole Tsh. 300,000/=, Masala s/o Mabula wa
eneo la Changombe Tsh. 70,000/= na Duka la Lazia Shop ambalo liko Mtendeni
Street Tshs 200,000/=.
Natoa wito kwa wamiliki na wakala
wote wanatoa huduma hizo kuwa makini wanapoendesha shuguli zao, kwa kutoa
taarifa za watu wanaowatilia shaka wanaofika kutaka huduma katika maduka yao
mara moja ili wakamatwe na kufikishwa katika vyombo vya sheria.
[D. A. MISIME – ACP]
KAMANDA WA POLISI [M] DODOMA
CONTACT:
POLISI MKOA WA
DODOMA
DAWATI LA HABARI, ELIMU NA
MAHUSIANO,
Phone:
0715 006523 – Luppy Kung’alo – Mrakibu msaidizi wa Polisi (ASP)
Phone:
0712 360203 – Silyvester Onesmo – Police
Konstebo (PC)
No comments:
Post a Comment