Habari za Punde

*KUNDI LA MCHIRIKU LA JAGWA MUSIC LINAVYOWAPAGAWISHA WAZUNGU, KUTOKA USWAHILINI HADI UGHAIBUNI

*Mchiriku wa Jagwa Music Kutoka Uswahilini uliovamia Ulaya ! 
*Wazungu wanapandishwa Mzuka na ukichaa na mchiriku wa Wabongo 
*Hakuna kisichowezekana katika maisha ! kila kitu kinawezekana,
Unapozungumzia muziki wa bongo katika viwanja vya kimataifa, wawakilishi au wasanii wetu kutoka uswahilini wanazidi kuongezeka na kuwageuzia kibao wazungu kwa kuwa mdundo ya ajabu inayowachengua akili washabiki, kama anavyosema kamanda wa harakati za kuitangaza Tanzania kimuziki mwanamuziki kamanda Ras Makunja wa FFU kuwa " from East to west Bongo is the best" na kauli hii ya kujiamini ya kamanda, ndio kama dira ya mfano hai inayowafanya Kikosi cha batariani cha JAGWA MUSIC (Mchiriku) kutoka Uswahilini jijini Dar-es-salaam, Kikundi cha muziki wa mchiriku Jagwa na mdundo wao umeanza kuzoeleka katika masikio ya maelefu ya washabiki ya wakazi wa ulaya.
Mdundo wa mchiriku wa Jagwa Music licha ya kuteka nyoyo za washabiki wa ulaya, wazungu wamekua hawayaamini macho yao pale wanapoliona kundi hilo jukwaani na yombo ambayo ni vya kinyeji na kinanda cha aina ya casio (cha watoto) lakini kinatoa mlio unawachezesha na kuwatia wazimu maelfu ya washabiki  ! hii haingii kabisa akilini mwa wazungu ! Kuona vijana kutoka uswahilini kabisa na mdundo wao "Mchiriku" kutoka Uswahilini na vyombo vya uswahilini unatingisha ulaya.
Vijana wa Jagwa Music (Mchiriku) wanakubalika kimataifa bila wasi wasi yeyote Jagwa Music wameshayatingisha majukwaa ya Ujerumani,Denmark,Sweden na Holland na CD zao zipo sokoni na kila wanapotumbuiza mauzo ya CD "bongo hotheads"  pesa zinaingia moja kwa moja wa wasanii hao bila ya longo longo.
Lakini bado tunajiuliza pamoja na wanamuziki wa Tanzania kutoka Uswahili wanaitangaza Tanzania je hapa nyumbani wanathaminika ? Kwa kwanini ? baadhi ya ngoma au mitindo ya kiasili ya kitanzania kama vile Ngoma ya Mdundiko ilipigwa marufuku, Ngoma za kinamama za kuwapa mafunzo wasichana kama vile "Unyago" , Msondo n.k zinauliwa na watanzania kupenda ulimbukeni wa utamaduni wa kigeni ?
Ninamatumaini kuwa wanamuziki wanao tuwakilisha nje ya nchi kama vile Jagwa Music,Ras Nas wa kule Norway, Kamanda Ras Makunja na Ngoma Africa band aka FFU, watapewa kipau mbele katika Tuzo za hapa nyumbani.
Acha tujirushe na "Mpango Mzima" wa Baba Dula 
Tembelea http://www.youtube.com/watch?v=wf7hWQ4FWDc kuapata uhondo zaidi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.