Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Richard Lusinga. A.K.A - Richie Mavoko (katikati) akizungumza na waandishi wa habari hawapo pichani leo katika Ukumbi wa Idara ya Habari MAELEZO, jijini Dar es Salaam, wakati akitoa shukrani kwa niaba ya Kampuni yake ya Aljazerra Entertaiment. Ambapo amesema kuwa " kama msanii wa kizazi kipya amewomba radhi kwa wote aliowakosea na yeye pia amewasemehe" Pamoja na Kushukuru kampuni ya Aljazerra Entertaiment, waandishi wa habari na wadau wote wa muziki nchini, kwani ndio waliomfikisha katika hatua aliyonayo kwa sasa, na kuahihidi kwamba atazidi kuboresha na kuwaletea nyimbo kali zaidi mashabiki wake na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya katika mwaka wa 2013.Richie Mavoko anatamba na nyimbo zake kama Mbona Silali,Follow Me,One Time na Marry Me . (kushoto ) Ni Msanii Mwanaisha Nyange (a.k.a DYANA).
Msanii wa kike anayechipukia katika tasnia ya muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Mwanaisha Nyange (a.k.a- Dyana) naye pia akizungumza na waandishi wa habari (hawapo) pichani wahakati wa hafla fupi ya kutoa shukrani kwa wadau wa muziki nchini, iliyofanyika leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Msemaji wa Aljazerra Entertaiment, Simon John.
Msanii Richie Mavoko (kulia), pamoja na Msanii Mwanaisha Nyange (kushoto) a.k.a- DYANA wakipozi kwa picha baada ya mkutano wao na waandishi wa habari leo. Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
No comments:
Post a Comment