Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya uzinduzi wa Barabara ya Mfenesini-Bumbwini Wilaya ya Kaskazini B Unguja jana. Barabara hiyo imejengwa na Kampuni ya Mecco kwa umefadhiliwa na Benki ya Dunia na Serikali ya Mapinduzi,ikiwa ni sehemu ya shamra shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,(katikati) Mwakilishi wa ADB Tanzania Toniya Kandiero,(wa pili kushoto) Naibu Waziri wa Mindombinu, Mawasiliano Issa Haji Gavu,(wa pili kulia) Katibu Mkuu wa Miundombinu,Mawasiliano,Dk.Juma Malik Akili,(kulia) na Mkuu wa Mkoa wa Kasakazini Unguja Pembe Juma,(kushoto) wakitembea katika Barabara ya Mfenesini-Bumbwini, baada ya kuifunguliwa rasmi jana,ikiwa ni sehemu ya shamra
shamra za kuadhimisha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar. Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
No comments:
Post a Comment