Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa akiongea na waandishi wa habari wakati wa kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road, kampeni iliyozinduliwa leo ikiendeshwa na kampuni ya Green Waste Pro ltd. yenye zabuni ya kusafika maeneo yanayoizunguka manispaa ya Ilala ambapo amesema zoezi hilo litadumu kwa wiki tatu mfululizo kwa Jumamosi ya kila wiki.
Mstahiki meya Jerry Silaa amewataka wananchi wa manispaa ya Ilala kujitokeza na kushiriki kikamilifu katika zoezi la kusafisha maeneo ya kata zao. Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi.
Pichani Juu na Chini Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala Jerry Silaa (kulia), Mh. John Chiligati ambaye ni mkazi wa Kivukoni na mkuu wa wilaya ya Ilala Bw. Raymond Mushi wakishiriki katika zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road leo jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akishiriki katika zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi iliyopo katika maeneo ya Ocean Road jijini Dar es Salaam ikiwa ni kampeni maalum ya kuweka mazingira safi katika maeneo mbalimbali yanayoizunguka Manispaa ya Ilala ambapo Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. imechekuza Zabuni ya kusafisha Manispaa ya Ilala na kata zake tatu.
Picha Juu na Chini ni Baadhi ya raia wa kigeni kutoka taasisi ya Roots and Shoots wakiunga mkono zoezi hilo na kuhakikisha manispaa Ilala inaongoza kwa usafi.
Picha juu na chini niVijana wa Ilala Jogging Club waliokuwa wakifanya mazoezi katika fukwe hiyo wakati zoezi la kufanya usafi likiendelea na kuamua kusitisha mazoezi yao na kushiriki na kujumuika kusafisha fukwe hiyo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo akiwajibika wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road jijini Dar.
Greda likifanya kazi ya kubeba takataka ngumu katika fukwe ya Ocean Road ambazo hazizoleki kwa mkono.
Lori la kubebea takataka la Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. likiwa limesheheni uchafu uliokusanywa wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi iliyopo maeneo ya Ocean Road jijini Dar.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Green Waste Pro Ltd. wakiwajibika wakati wa zoezi hilo.
Afisa Usafishaji wa Manispaa ya Ilala Bw. Samuel Bubegwa (kushoto) akiwa na mdau wakati za zoezi hilo.
Kutoka kulia ni Bw. Said Mazingira, Afisa Habari wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd Bi. Vidah Fammie, Meneja Mkuu Bi. Elizabeth, Operation Manager Bw. Abdallah, Cindy na Mdau wa kujitolea Joshua wakionyesha Umoja wakati wa zoezi la kusafisha fukwe ya bahari ya Hindi.
Mstahiki Meya Jerry Silaa akiwashukuru vijana wa Ilala Jogging Club kwa kushiriki zoezi la kusafisha fukwe hiyo na kuwataka waendelee na moyo huo kwa maana suala la usafi ni letu sote.
Baadhi ya wakazi wa Kata ya Kivukoni walioshiriki zoezi la usafi wa fukwe ya bahari ya Hindi iliyopo maeneo ya Ocean Road jijini Dar.
Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Green Waste Pro Ltd. Bw. Anthony Mark Shayo (kushoto) akivuta pumzi na wadau waliojitokeza kushiriki zoezi la kusafisha fukwe za bahari ya Hindi.
Baadhi ya wafanyakazi wa Green Waste Pro ltd, wadau na wananchi wakipangiana maeneo ya kufweka majani katika fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road.
Mmoja wa wakazi wa jijila Dar anayefanya shughuli za kukusanya chpa za maji akionekana kufurahia mazingira hayo kuwa safi na kuamua kuweka kiroba chake chini na kumpumzika katika fukwe hiyo.
Moja ya Sehemu ya Fukwe ya bahari ya Hindi maeneo ya Ocean Road iking'ara baada ya kufanyiwa usafi.
No comments:
Post a Comment