Katibu
wa Simba, Evodius Mtawala akimwongoza kocha mpya wa klabu hiyo, mfaransa Patrick
Liewing, wakati alipowasili kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius
Nyerere, Dar es salaam, akitokea Ufaransa. Kocha huyo atarithi mikoba ya Milovan, aliyetimuliwa na timu hiyo mara tu baada ya kumalizika kwa mzunguko wa kwanza wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara, ambapo sasa kocha huyo atakuwa na kibarua kigumu kwa kuwahakikishia mashabiki wa timu ya Simba kuwa yeye ni zaidi ya Milovan na kuonyesha kile kilichowafanya viongozi wa Simba kumtimua Milovan na kumkaribisha yeye, ambapo ataanzia katika Kombo la Mapinduzi linalotarajia kuanza hivi karibuni mjini Zanzibar.
Rais Samia amwomba Drogba kuwa Balozi wa Tanzania AFCON 2027
-
RAIS Samia Suluhu Hassan amemuomba mshambuliaji wa zamani wa timu ya taifa
ya mpira wa miguu ya Ivory Coast na Chelsea ya England, Didier Drogba kuwa
Bal...
13 hours ago

No comments:
Post a Comment