Waziri wa
Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Dkt.
Fenella Mukangara (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu Waziri wa Sheria na
Katiba, Angellah Kairuki (katikati) pamoja na Mbunge wa Viti maalumu Ester Bulaya, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, leo.
Mwanasheria Mkuu Mkuu
wa Serikali Mh. Jaji Frederick Werema (kulia) akibadilishana mawazo na Naibu
Wazir wa Habari,Vijana, Utamaduni na Michezo, Amos Makalla, leo Bungeni mjini
Dodoma.
Waziri wa Katiba na Sheria Mathias Chikawe (kulia)
akizungumza na Mbunge wa Korogwe Mjini, Yusuph Abdallah Nassir, katika viwanja vya Bunge mjini Dodoma, leo.
Mbunge wa Iramba
Magharibi Mwingulu Nchemba (kulia) akizungumza na Mbunge wa Arumeru Mashariki kupitia CHADEMA, Joshua Nasari, kwenye viwanja vya Bunge mjini Dodoma, leo.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa (kushoto), Mbunge wa Viti Maalumu, Margaret
Sitta (wa pili kushoto) na
Waziri wa fedha William Mgimwa (mwenye miwani) pamoja na Mbunge wa kuteuliwa
James Mbatia (kulia) wakibadilisha mawazo nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma
leo , baada ya Mbunge James Mbatia kuwaslisha hoja yake binafsi
kuhusu Udhaifu uliopo katika sekta ya Elimu nchini.
Waziri wa Elimu na
Mafunzo ya Ufundi, Shukuru Kawambwa, akionyesha kimoja kati ya vitabu vinavyotumika
mashuleni alipokuwa akijibu hoja mbalimbali
zinazohusu elimu baada ya Mbunge wa kuteuliwa wa NCCR- Mageuzi, James Mbatia, kuwakilisha hoja yake binafsi ya
Udhaifu uliopo katika sekta ya elimu nchini. Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO
No comments:
Post a Comment