Habari za Punde

*LULU APEWA DHAMANA, JE KWA SASA KUWA NJE NI SALAMA?


Mahakama Kuu ya Tanzania,  imemwachia kwa dhamama msanii Elizabeth Michael 'Lulu', aliyekuwa akikabiliwa na kesi ya kudaiwa kuuwa bila kukusudia,  msanii mwenzake Steven Kanumba, mwaka jana.


Lulu amepewa dhamana hiyo baada ya Makama kupitia vifungu kadhaa na kuona kesi yake ya kuua bila kukusudia inamruhusu kupewa dhamana.

Msanii huyo ambaye anatuhumiwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake, Steven Kanumba - The Great, alibadilishiwa kosa la kuua na kuwa kuua bila kukusidia, ambalo, kwa mujibu wa sheria linadhamnika na kwamba ikiwa mtuhumiwa atapatikana na hatia, adhabu ya juu kabisa ni kifungo cha maisha, miaka kadhaa au kuachiwa huru
Msanii Lulu wakati akiwa Mahakamani leo asubuhi alipokuwa akisomewa taratibu za dhamana yake, ambapo kwa upande wa Mawakili wa Serikali walisema kuwa hawana pingamizi na dhamana hiyo. Picha na Emmanuel Shilatu blog. 

Ikumbukwe kuwa Msanii huyo aliwahi kuomba ruhusa ya kuhudhuria mazishi ya rafikie kipenzi, Steven Kanumba, kwenye mazishi yake, wakati alipokuwa rumande, lakini kwa kuhofia usalama wake vyombo husika viligoma na kuelezea kuwa usalama wake utakuwa hatarini.

Sasa je kwa kupewa dhamana msanii huyo hivi sasa ataweza kuishi kwa amani mtaani kama alivyozoea? na je atahakikishiwa usalama wake popote aendako? na vipi familia yake imejiandaaje kumlinda kwa kipindi hiki atakapokuwa nje kwa dhamana? hayo ni miongoni mwa maswali yanayotawala vichwani kwa wanaoliangala jambo hili kwa jicho la tatu.

Inaaminika wananchi walio wengi, mashabiki wake na wengineo wana hamu sana ya kumuona akiwa nje na walikuwa wakimuonea huruma sana msanii huyo kwa kile kilichomkuta, lakini kwa sasa ni jukumu la kila mmoja wetu aliye karibu na msanii huyu, na hata kila mmoja kwa wakati wake kumlinda msanii huyu kwa njia yeyote ile ili asijekutimia ile sehemu ya maneno yake wakati akiwa rumande, kwa kufanya lolote kwa kuogopa maneno ya wanajamii.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.