Habari za Punde

*MeTL GROUP YADHAMINI MBIO ZA MARATHON ZA KILOMETA 10 USIKU WA MKESHA WA MWAKA MPYA JIJINI DAR

Mwandaaji wa Mashindano ya Marathon ya Kilomita 10 ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 ambapo amewashukuru Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Kwa kudhamini mashindano kama haya kwa sababu miaka ya nyuma yalikuwa yakikosa udhamini wa kuaminika na kwa mshangao wa wengi walikua wakijua Mohammed anadhamini Soka tu lakini hawajui kwamba hachagui na anadhamini michezo yote.

Kutokana na udhamini wake sasa tumepata mahali pakujenga uwanja wa Riadha kwa sababu Uwanja wa Taifa sasa umekuwa kama uwanja wa maonyesho wa soka lakini riadha tunakusudia kujenga Pwani.
Mwandaaji huyo amemshukuru mdhamini wa michezo hiyo na kusema kwamba wao kama chama watatimiza malengo ya chama hicho kuitangaza Tanzania Kimataifa katika riadha.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bw. Anthony Mtaka akizungumza na waandishi wa habari ambapo ameshukuru ubunifu huu wa kuazimisha mkesha wa mwaka mpya kwa aina tofauti ambapo watu wengi wamezoea kuadhimisha katika kumbi mbalimbali za burudani lakini sisi tumeadhimisha mwaka mpya kimichezo zaidi kwa kufanya Marathon ya Kilometa 10 yaliyojulikana kama MeTL New Years Eve Midnight Race.

Sisi kama wanamichezo tumekubaliana na wazo hili la kufanya Marathon kama hii na tumashukuru MeTL GROUP kwa kudhamini kitu kama hichi cha kipekee n kuwataka washiriki wajitokeze kwa wingi mara nyingine na pia huu usiwe mwisho bali uwe ni mwanzo wa kuendeleza michezo Tanzania na tunakiomba chama cha Riadha RT kushirikiana na wadau wa michezo kukuza mchezo wa riadha Tanzania.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiambatana na viongozi wa chama cha riadha Tanzania RT kuelekea kuzindua rasmi mashindano ya riadha ya Kilomita 10 yaliyofanya maeneo ya Masaki jijini Dar na kumalizika katika Polisi Officers Mess.
Washiriki kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania wakiwa wamejipanga tayari kuanza mbio za Marathon 2012 katika mkesha wa mwaka Mpya jijini Dar es Salaam.
On your Mark...........Get Ready.......Paaaa..... Mgeni rasmi Bw. Anthony Mtaka aliyenyanyua mkono juu kufyatua baruti kuashiria kuanza rasmi kwa mbio hizo huku washiriki nyuma yake wakijipanga kushindana vilivyo.
Mshindi wa kwanza katika mbio hizo kwa upande wa Wanaume Bw. Dickson Marwa akimaliza mbio hizo kwa kutumia muda wa 29:14:45.
Baadhi ya washiriki wengine wakimaliza ngwe ya mashindano hayo ya Kilometa 10 yaliyomalizika katika bwalo la polisi Masaki Jijini Dar es Salaam.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania L.t.d (MeTL GROUP) Bw. Cosmas Mtesigwa akichezea ngoma za asili ya kabila la Wagogo sambamba na Watumbuizaji hao wakati wa mashindano ya riadha ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' usiku wa mkesha wa Mwaka mpya 2013 yaliyofanyika usiku wa kuamkia leo Masaki jijini Dar.
Pichani juu na chini washiriki walifanikiwa kumaliza mbio hizo wakijiandikisha.
Joggers wakiingia katika viwanja vya Police Officers Mess baada ya kumaliza ngwe yao katika mashindano hayo ya mbio za kilomita 10 yaliyodhaminiwa na Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL GROUP) katika mkesha wa kuukaribisha mwaka mpya 2013 usiku wa kuamkia leo.
Mmoja wa washiriki wa mbio hizo Bw. Said Abrahman kutoka Zanzibar akiwa amezinduka baada kuzimia alipo maliza ngwe hiyo katika viwanja vya Police Officers Mess jijini Dar es Salaam.
Meza Kuu...Mwakilishi kutoka kampuni ya MeTL GROUP Bw. Cosmas Mtesigwa akiteta jambo na Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka kabla ya kuanza kwa zoezi la kutoa zawadi kwa washindi.
Pichani juu na Chini ni Baadhi ya washiriki wa Marathon wakicheza kwaito na kufurahia baada ya kutimia saa 6 kamili na kuuona mwaka Mpya 2013.
Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akiwa na waratibu wengine wa shindano hilo wakiratimisha shindano hilo ili kujua kuweza nani amepata pointi zipi na kuweza kumtangaza mshindi halali.
Pichani Juu na Chini ni Mgeni rasmi Rais wa Shirikisho la Riadha nchini Tanzania Bw. Anthony Mtaka akiongoza washiriki mashindano ya riadha na wageni waalikwa kupata chakula cha jioni kabla ya kukabidhi zawadi kwa washindi.
Rais Mstaafu wa Chama cha Riadha nchini (RT) Bw. Francis John akitoa nasaha kwa washirki ambapo amewataka kuongeza juhudi zaidi na kutokata tamaa kwa kuwa michezo ni Afya na kuwaasa wananchi wengine zaidi kujitokeza pamoja na wadhamini wengine katika tukio kama hili ili kuupa kipaumbele mchezo wa Riadha kama ilivyoonyesha mfano na kampuni ya MeTL GROUP.
Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akiwatolea uvuvi viongozi wa vyama vya michezo vya sasa kuwacha kula kwenye michezo ya wanamichezo na kujikita katika kuvumbua vipaji vipya kwa sababu tumekuwa tukiwaona walewale kila siku kwa kufanya hivyo mtakuwa hamkuzi mchezo huu.
Mwakilishi wa Kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Ltd (MeTL GROUP) Bw. Cosmas Mtesigwa akizungumza kwa niaba ya Kampuni ambapo imeahidi kuendelea kushirikiana na wabunifu wa michezo hii na pia kuendelea kushirikiana nao bega kwa bega mpaka kufikia michezo ya Olimpiki itakayofanyika mjini Brazil na kuhakikisha wanapata medali na kuipatia sifa nchi yetu kwa kuwa na wanamichezo bora.
Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akiwaasa washiriki na kutoa shukrani za pekee kwa Kampuni ya MeTL GROUP kwa kuelekeza macho nguvu zao kusapoti mchezo wa riadha ambao umekuwa haupewi kipaumbele na wadhamini wengine ambao wamekuwa wakitazama mchezo wa mpira wa miguu na michezo mingineyo.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Bw. Dickson Marwa aliyemaliza katika muda wa dakika 29:14:45 zilizodhaminiwa na MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw. Francis John.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya kitita cha Shilingi 500,000/= kwa mshindi wa kwanza kwa upande wa wanaume wa mashindano ya 'MeTL New Years Eve Midnight Race' Bi. Sara Ramadhani aliyemaliza katika muda wa dakika 33:02:31 zilizodhaminiwa na MeTL GROUP. Kulia ni Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. Bw. Cosmas Mtesigwa na Kushoto ni Mwandaaji wa Mashindano hayo Sarah Ramdhani ambaye pia ni mchezaji na amewahi kukiongoza chama cha Riadha Tanzania kwa miaka 10 akifuatiwa na Mwenyekiti mstaafu wa chama cha riadha Tanzania Bw. Francis John.
Mwakilishi kutoka kampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited. (MeTL) Bw. Cosmas Mtesigwa akikabidhi zawadi ya kitika cha Shilingi 100,000/= kwa Mshindi wa tatu kwa jamii ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw. Mathia Jolo aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika 43:16:07 yaliyofanyika katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers Mess jijini Dar es Salaam
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikabidhi zawadi ya kitika cha Shilingi 500,000/= kwa Mshindi wa pili kwa jamii ya watu wenye ulemavu walioshiriki mashindano hayo Bw. Shukuru Khalfan aliyemaliza mbio hizo za Kilometa 10 kwa dakika 38:51:10 yaliyofanyika katika mkesha wa Mwaka mpya 2013 Police Officers Mess jijini Dar es Salaam.
Mgeni Rais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka ( wa pili kulia) akikata keki ya kuukaribisha na mwaka 2013 baada ya kukabidhi zawadi kwa washiriki wa Marathon za Mbio za Kilometa 10 usiku wa kuamkia leo jijini Dar.
MgeniRais wa Chama cha Riadha Tanzania (RT) Bw. Anthony Mtaka akifungua rasmi muziki kwa wote baada ya zoezi la kukabidhi zawadi.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.