Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizungumza wakati wa hafla maalumu ya kuwakaribisha wake wa Balozi nchini kwa mwaka mpya 2013, Hafla hiyo ilifanyika katika viwanja vya Ikulu jijini Dar- es Salaam , Jana.
Baadhi ya wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zaoTnzania wakisubiri kuanza kwa hafla ya kukaribisha mwaka mpya 2013 katika viwanja vya Ikulu jjijini Dsm Jana, hafla hiyo iliandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (hayupo pichani).
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akiongozana na mke wa Makamu wa Rais, Mama Asha Bilal, wakati wakiwasili eneo la tukio kwenye hafla hiyo ya kuwapongeza wake wa Mabalozi.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (kushoto) akibadilishana mawazo na Mke wa Waziri Mkuu Mama Tunu Pinda, katika hafla maalumu ya mwaka mpya 2013 kwa ajili ya wake wa Mabalozi iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete kwenye viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto) akipongezana na Consulate wa Jamhuri ya Poland Bibi Grazyna Tairo,wakati wa hafla hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akipongezana na Kiongozi wa wenza wa Mabalozi nchini Celine Khalfan Juma Mpango katika hafla hiyo.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (mwenye kilemba) akibadilishana mawazo na baadhi ya wake wa Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wakati wa sherehe ya hafla ya kuukaribisha mwaka 2013 katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam,jana.
Mke wa Makamu wa Rais Mama Asha Bilal (aliyekaa) akisalimiana na Msaidizi Mwandamizi wa Rais masuala ya Diplomasia, Liberata Mulamula, walipokutana katika hafla ya kusherehekea mwaka mpya 2013 kwa ajili ya wake wa Mabalozi nchini iliyoandaliwa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete katika viwanja vya Ikulu jijini Dar es Salaam Jana.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete (kushoto)akisalimiana na Mdau Fauzia Aboud, katika hafla hiyo katika viwanja vya Ikulu jijini Dar e Salaam Jana.Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO.
No comments:
Post a Comment