Rais wa Shirikisho la Ngumi la Kimataifa IBF bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati, Mtanzania Onesmo Ngowi atakuwa msimamizi mkuu wa mapambano ya ubingwa wa yatakayofanyika nchini Ghana tarehe 8 na 30 March 2013.
Mapambano hayo ni yale yanayowakutanisha mabondia Richard Commey akipambana na Mgana mwenzake Bilal Mohammed wakigombea mkanda wa IBF Afrika na Ghuba ya Uajemi (IBF AMEPG) katika uzito wa Lightweight. Mabondia wote wawili wana rekodi zinazovutia, Commey ana makazi yake katika jiji la London nchini Uingereza.
Mpambano wa pili siku hiyo utawakutanisha mabondia wawili wa Ghana Fredrick Lawson akipambana na bondia machachari Isaac Sowah. Wote wanaishi nchini Ghana.
Mapambano yote yatafanyika wakati bingwa wa dunia wa zamani wa IBF Joseph Agbeko atakapochuana na bondia Luis Melendez wa Mexico kugombea ubingwa wa dunia wa IBO katika uzito wa bantam.
Mpambano mwingine ambao Ngowi atasimamia ni kati ya bondia Helen Joseph wa Nigeria na Fatuma Zarika wa Kenya ambao watagombea mkanda wa IBF wa mabara wa wanawake. Helen Joseph ni mkazi wa Ghana wakati Fatuma Zarika anaishi nchini Ujerumani.
Maofisa wengine watakaomsaidia Ngowi katika mapambano hayo ni pamoja na: Refarii: Rodger Barnor, Jaji namba 1 ni Fred Ghartey, Ghana, Jaji namba 2 ni Confidence Hiagbe na jaji namba 3 ni May Mensah Akakpo, Ghana
Mapambano haya ni kati ya mapambano 100 ambayo IBF imepania kuyafanya katika ukanda wa Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati mwaka huu 2013.
Imetolewa na:
UTAWALA:- International Boxing Federation Africa
Dar-Es-Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment