Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Ali Iddi (wa tatu kushoto) akifurahia pamja na Nahodha wa timu ya Azam Fc, Himid Mkami na Jabir Aziz, baada ya kuwakabidhi zawadi ya kitita cha fedha taslimu Sh. Milioni 10, na Kikombe cha ushindi baada ya kuifunga timu ya Tusker ya Kenya kwa mabao 2-1, katika mchezo wa Fanali ya Kombe la Mapinduzi zilizofikia tamati, jana Januari 12, huku mshindi wa pili wa mashindano hayo, Tusker ya Kenya wakijipatia kiasi cha Sh. Milioni 5 na Kikombe cha mshindi wa pili, na zawadi ya mfungai Bora wa michuano hiyo alikuwa ni Mchezaji wa Tusker ya Kenya, Jese Wele, aliyejinyakuliwa Sh. 300,000.
Mchezaji wa Azam Fc. Gaudance Mwaikimba (katikati) akiruka kuwania mpira na kipa wa Tusker ya Kenya, Samuel Odhiambo, wakati wa mchezo wa Kombe la Mapinduzi. Bao lililofungwa na Mwaikimba katika Dakika ya 93 ndani ya muda wa dakika za nyongeza, liliiwezesha timu hiyo kuwa mabingwa wa Kombe la Mapinduzi kwa mara ya pili mfululizo.
Mwaikimba, akikosa bao la wazi......., Katika mchezo huo timu ya Tusker ndiyo ilikuwa ya kwanza kujipatia bao lililofungwa na Jese Wele, katika Dakika ya 60, na baadaye Azam waliweza kusawazisha bao hilo kupitia kwa Beki wake, Jockins Attudo, kwa njia ya penati katika dakika ya 72, baada ya mchezaji mmoja wa Tusker kuunawa mpira katika eneo la hatari kufuatia shuti kali lililopigwa na Khamis Mcha.
Beki na Nahodha wa Azam, Himid Mkami, akijipinda kupiga shuti wakati akiokoa moja ya hatari zilizoelekezwa langoni kwake.
Kipa wa Tusker ya Kenya, Samuel Odhiambo, akigaa gaa chini, baada ya kushindwa kuokoa mkwaju wa penati, iliyopigwa na Attudo.
Shughuli ilikuwa pevu kati ya Mwaikimba na Shikokoti, Hapa Mwaikimba akijipinda kuachia shuti ambalo hata hivyo halikuweza kuzaa matunda.
'KITUKO UWANJANI' Aidha katika mchezo huo kilizuka kituko cha mwaka, baada ya mwanadada huyu aliyevalia ushungi kukatika katikati ya uwanja wakati mchezo ukiendele, jambo ambalo lilimfanya mwamuzi wa mchezo huo, kusimamisha mchezo na kumfuata ili kujua kulikoni. Hapa ni wakati akilia denge ili amzuie asikatize uwanjani, lakini hakufanikiwa kwani kila alivyojitahidi kumsihi mdada huyo, hakusikilizwa ila mdada huyo aliendelea kwenda kuelekea kukatiza uwanjani hapo, jambo ambalo lilizua hisia nyingine miongoni mwa mashabiki wa soka waliokuwepo uwanjani hapo huku, yakisikika makelele ya mshangao kutoka majukwaani.
Mwamuzi akizungumza na mdada huyo huku akitumia busara umsindikiza nje ya uwanja....
Bado hakijaeleweka....
Mwamuzi huyo baada ya kuona amemfikisha salama na kuvuka alama ya mstari wa mwisho wa uwanja, alianza kuomba msaada wa askari ili kumtoa bonti huyo uwanjani.
Binti huyo akiwa tayari chini ya ulinzi wa polisi, huku akisindikizwa na Msemaji wa Kamati ya Maandalizi ya mashindano ya Kombe la Mapinduzi, Farouk Kareem.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akimkabidhi zawadi ya Kombe la mshindi wa pili, Nahodha wa Timu ya Tusker kutoka Kenya, Joseph Shikokoti, baada ya timu yake kukubali kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Azam, katika mchezo uliochezwa kwenye Uwanja wa Amani, mjini Zanzibar jana usiku.
Makamu wa pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Iddi, akimkabidhi zawadi ya Sh. 300,000, mfungaji bora wa mashindano hayo, Jese Wele.
Gaudance Mwaikimba, akifurahia kombe na mashabiki wa timu hiyo.
No comments:
Post a Comment