Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, akizungumza na wanachama wa Nungwi Saccos, wakati alipofika kutembelea kikundi cha Ushirika cha Kinamama, kilichopo Tawi la CCM Nungwi, kwa ajili ya kukabidhi ahadi ya mchango wa mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Salma kikwete, kiasi cha Sh. 2,000,000/- kwa kikundi hicho, jana.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, Mkurugenzi Tiba Dr. Salhia Ali Muhsin na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi, wakifurahia na kuangalia vifaa mbali mbali walivyovitoa kwa ajili ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Wilaya ya Kaskazini “A”, jana.
Mke wa Rais wa Zanzibar, Mwanamwema Sehni, akikabidhi Viti vya Wagonjwa kwa Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Dr. Salhia Ali Muhsin, wakati alipotembelea katika Hospitali ya Kivunge Wilaya ya Kaskazini A, jana.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, akionyesha kitita cha fedha, kuashiria utekelezaji rasmi wa ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Slma Kikwete ya kukabidhi mchango wa shilingi 2,000,000/- Ushirika wa Nungwi Saccos.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, akikabidhi mchango wa shilingi 2,000,000/- kwa kiongozi wa kikundi cha Nungwi Saccos, ikiwa ni utekelezaji wa ahadi ya Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano Mama Slma Kikwete aliyoitoa mwezi Mei mwaka 2010.
Akina mama wa Ushirika wa Nungwi Saccos wakishangiria mchango wa shilingi milioni 2,000,000/- zilizotolewa na Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni ambazo ziliahidiwa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete wakati akiizindua Nungwi Saccos Mwaka 2010.
*****************************************
SERIKALI ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuunga mkono juhudi za Wananachi wake katika kuhakikisha changamoto pamoja na matatizo yanayowakabili Wananchi hao yanatekelezwa.
Utekelezaji huo utaendelea kufanywa kwa pamoja kati ya Serikali, Taasisi na mashirika hisani kwa kuwajumuisha na wananchi wenyewe kutegemea nguvu na uwezo unavyoruhusu kiuwezeshaji.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni akiambatana na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman pamoja na wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM alitoa kauli hiyo mara baada ya kukabidhi misaada wa mbali mbali kwa ajili ya Hospitali ya Kivunge iliyoko Wilaya ya Kaskazini A.
Msaada huo uliogharimu jumla ya Shilingi Milioni Sita { 6,000,000/- } ukijumisha magodoro 16, Vitanda 16, Mito 16, Viti vya wagonjwa vitatu, Sabuni unafuatia ziara ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyoifanya katika Hospitali hiyo mwaka jana na kuelezewa changamoto kadhaa zinazoikabili Hospitali hiyo ikiwemo uchakavu na uhaba wa Vitanda na Magodoro.
Mama Mwanamwema Sheni aliwataka Wananachi na wafanyakazi wa Kituo hicho kuendelea kuwa wastahamilivu licha ya kwamba matatizo hayo ni kilio cha muda mrefu.
“ Upungufu wa Vifaa umekuwa ukizikumba Taasisi na majengo kadhaa ya Umma, Jamii na hata binafsi lakini cha kuzingatia zaidi ni ustahamilivu na kutafuta mbinu mbadala za kukabiliana na matatizo hayo”. Alisisitiza Mama Mwanamwema Sheni.
Mwenyekiti huyo wa Umoja wa wake wa Viongozi wa CCM aliikumbusha Jamii kuendeleza upendo na mshikamano kwa lengo la kulijengea hatma njema ya Amani na Utulivu Taifa hili.
Akipokea Msaada huo Mkurugenzi Tiba Wizara ya Afya Dr. Salhia Ali Muhsin alimpongeza Mama Mwanamwema Sheni pamoja na Wanachama wa Umoja huo wa Wake wa Wawakilishi na Wabunge wa CCM kwa juhudi zao za kusaidia maendeleo ya Jamii na Hasa wakilenga zaidi akina mama.
Baadaye Mama Mwanamwema Sheni alikabidhi Mchango wa Shilingi Milioni mbili { 2,000,000/- } kwa ajili ya Nungwi Saccos ili kutekeleza ahadi iliyotolewa na Mke wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete.
Ahadi hiyo ilitolewa na Mama Salma Kikwete wakati akiizindua Nungwi Saccos Tarahe 11 mwezi Mei Mwaka 2010 hapo katika Majengo ya Skuili ya Amali yaliyopo Mkokotoni Mkoa wa Kaskazinin Unguja.
Mama mwanamwema Sheni katika kuunga mkono juhudi wanazochukuwa wanachama hao za kujiletea maendeleo yeye pamoja na Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi wameahidi kuchangia Mabati kwa ajili ya Uwezekaji wa Jengo la Ushirika huo.
Aliwataka akina mama wote Nchini kudumisha mshikamano utakaosaidia Taifa kuendelea kupiga hatua kubwa zaidi za kiuchumi na ustawi wa Jamii.
Naye Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi akitoa nasaha zake katika hafla hiyo alieleza misaada hiyo ni miongoni mwa utaratibu ulioandaliwa na Umoja wa wake wa wawakilishi na Wabunge wa CCM.
Mama Asha alisema kwamba michango hiyo wakati wote hulenga katika kuunga mkono harakati zao za kiuchumi bila ya kuingiza itikadi za Kisiasa ambazo zimekuwa na utaratibu wa kulenga watu na makundi Maalum.
Akitoa Taarifa fupi Katibu wa Ushirika huo wa Nungwi Saccos Bibi Siti Ali Makame kwa niaba ya Wanachama wenzake wamewapongeza Viongozi wa Serikali na Taasisi zake kwa juhudi kubwa inazochukuwa katika kuona kundi kubwa la wanawake linakomboka katika dimbwi kubwa la umaskini.
Bibi Siti alisema wanachama wa kikundi hicho wametoa shukrani za pekee kwa Taasisi ya Kimataifa ya misaada ya Action Aid kutokana na jitihada zake zilizochangia kuanzishwa kwa ushirika huo wa Nungwi Saccos.
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Sheni, Mke wa Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mama Asha Suleiman Iddi pamoja na wake wa wawakilishi na wabunge wa CCM walipata wasaa wa kumtembelea Muasisi wa Chama cha Afro Shirazy Party Bibi Kombo Juma.
Ujumbe huo ulimjulia hali Muasisi huyo hapo nyumbani kwake katika Kijiji cha Nungwi kiliopo Wilaya ya Kaskazini “A” Mkoa wa Kaskazini Unguja
Imetolewa na Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
3/1/2013.
No comments:
Post a Comment