Mshambuliaji wa Simba, Mrisho Ngassa (kushoto) akimtoka beki wa African Lyon, Mussa Mude, wakati wakati wa mchezo wa fungua dimba mzunguko wa pili wa Ligi Kuu ya Vodacom, iliyoanza leo kati ya timu hizo kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam. Mpaka sasa Simba inaongoza kwa mabao 3-0 ambapo mabao ya Simba yamefungwa na Ramadhan Chombo Ledondo, katika dakika ya 3, na mabao 2 yakifungwa na Mrisho Ngassa, katika dakika ya 19 na 39. African Lyon, walikosa penati katika dakika ya 32 iliyopigwa na Shamte Ally.
Ni heka heka katika lango la African Lyon. Wakati huo huo huko katika uwanja wa Chamanzi, Azam Fc inaongoza kwa mabao 2-0 na viwanja vyote hivi sasa ni kipindi cha pili.
No comments:
Post a Comment