Baada ya miaka kadhaa inawezekana baadhi ya visiwa kama hivi kutoonekana kabisa kutokana na kuendelea kuliwa kila kukicha na kupotea kabisa, na hii kwa namna moja ama nyingine husababishwa na uharibifu wa mazingira na uharibifu wa vyanzo vya mito, misitu nk. Visiwa hivi ni miongoni mwa Visiwa vilivyopo Bahari ya Hindi katikati ya Dar es Salaam na Zanzibar, ambavyo vingi vionaonekana kuwa tayari vimekwisha potea kwa kufunikwa kabisa na maji huku vingine vionekana kuendelea kuliwa siku hadi siku.
Hiki ni moja kati ya visiwa vidogo vilivyokwisha liwa kabisa na kufunikwa na maji, ambapo siku za usoni hata alama hii ya kuwepoe kwa kisiwa mahala hapa itatoweka.
Na hiki pia ni moja kati ya visiwa vinavyoendelea kulika siku hadi siku....
Huu ni mmoja kati ya miamba iliyokwisha funikwa na maji baharini.......
Hiki nacho kama kinavyoonekana kikiwa nama kimepachikwa tu yaani kikiwa kimebaki kimening'inia.....
Uvamizi wa eneo la misitu kama hili na kuweka makazi kwa kujenga bila mpangilio ni moja kati ya tatizo kubwa la uharibifu wa mazingira, kama zinavyoonekana nyumba hizi zikiwa zimejengwa katika msitu huu uliopo pembezo ni mwa Bahari ya Hindi eneo la Zanzibar.
No comments:
Post a Comment