KOCHA
Mkuu wa klabu ya Yanga, Ernest Brandts amesema timmu yake itafanya vizuri katika
mechi ya marudiano ya kirafiki dhidi ya Black Leopards ya Afrika Kusini
niliyopangwa kufanyika kesho (Jumatano) mjini Mwanza.
Brandts
alisema wachezaji wake wote wamefikia kiwango kile anachotaka na mchezo huo
utakuwa muhimu sana kwake kwani ni wa mwisho kabla ya kuingia katika kampeni za
kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara.
Alisema
kuwa Black Leopards ni timu nzuri na walipata mazoezi mazuri katika mechi ya
kwanza iliyofanyika kwenye uwanja waTaifa jijini na kushinda kwa mabao
3-2.
“Ni
mechi nzuri ambayo nadhani itakuwa ni kipimo kikubwa kabla ya kuanza kwa LigiKuu
ya Tanzania Bara, wachezaji wangu wana viwango vizuri sana kwa
sasa na naamini makosa yaliyofanyika katika mechi ya kwanza hawatayafanya tena,”
alisema Brandts.
Kuhusiana
na mabacha wawili, Mbuyu Twite na Kabanga Twite kucheza upande wa
kulia, Brandts alisema kuwa wachezaji hao wana uwezo wa kucheza nafasi nyingi
katika timu yake na uamuzi huo ulikuwa na faida kwa Yanga.
“Kabanga
anauwezo wa kucheza nafasi ya ushambuliaji, katikati, beki zote na hata Mbuyu
ana uwezo huo, hivyo uwepo wao katika timu ni mkubwa, niliwapumzisha kutokana na
mipango ya mechi na wala si vinginevyo,” alisema.
Msemaji
wa Klabu Yanga, Baraka Kizuguto alisema jana kuwa pamoja na mechi hiyo kuwa ya
maandalizi ya Ligi Kuu ya Tanzania Bara, pia wameamua kuicheza ili kuwapa
burudani mashabiki wa Mwanza.
Kizuguto
alisema kuwa Yanga haitakuwa na mechi yoyote katika mzunguko wa pili Kanda ya
ziwa na hiyo ndiyo nafasi yao ya kuwapa waonyesha uwezo wao mkubwa mashabiki wa
Mwanza nini wamekipata kutoka Uturuki.
“Tuna
mashabiki wengi sana Mwanza na Kanda ya Ziwa kwa ujumla, hii ni fursa kwetu
kwani mahsbaiki na wanachama watapata fursa ya kuona kiwango na maandalizi ya
timu yao kabla ya kuanza kwa mzunguko wa pili,” alisema Kizuguto
No comments:
Post a Comment