Habari za Punde

*MAMA JASIRI AKOMAA NA ALIYEMWIBIA MKOBA WAKE NA KUMPELEKA MWENYEWE KITUONI

 Mama ambaye hakuweza kufahamika mara moja jina lake, akimrushia konde zito jamaa aliyedaiwa kumwibia mkoba wake mama huyo, uliokuwa na pesa, simu pamoja na Paspoti ya kusafiria ya mumewe anayeonekana pichani (wa pili kulia). Imeelezwa kuwa mama huyo alikuwa amenasa katika kijimtaro eneo la Kituo cha Samaki Mbezi Beach jana usiku majira ya saa nne, na kuamua kuomba msaada wa kunasuliwa gari yake katika eneo hilo kutoka kwa waendesha Pikipiki 'Boda Boda' waliokuwa wakisubiri abiria kituoni hapo. 

Imeelezwa kuwa baada ya kuoba msaada walijitokeza vijana kutoka miongoni mwa waendesha pikipiki hao na kumnasua mama huyo wakisaidiana na mumewe, lakini baada tu ya kufanikisha zoezi hilo mmoja wao aliingiza mkono katika dirisha la nyuma na kuchukua mkoba na kisha kuanza kukimbia nao huku mume wa mama huyo akijitahidi kuwakimbiza bila mafanikio, huku jamaa huyu aliyekamatwa akisikika kuwatetea jamaa hao, akisema, 'achana nao hao mimi nawafahamu', ndipo mume wa mama huyo alipoamua kuruachana nao kwani walivuka barabara na kutokomea goizani upande wa pili wa barabara na kurudi kuanza kumuuliza vizuri jamaa huyo ili waweze kufanya taratibu za kuwapata. 

Ghafla jamaa huyo alianza kukana kuwa hawafamu, ndipo songombingo ilipoanza kwani mume na mke waliamua kumng'ang'ania jamaa huyo huku wakisaidia na baadhi ya waendesha pikipiki waliokuwa eneo hilo hadi walipofanikiwa kumpandisha katika gari yao na kuelekea naye kituoni.
 Shughuli ya kumdhibiti ikiendelea.
 Mama huyo akiendelea kumdhibiti jamaa huyo kwa kumpiga tanganyika jeki.
Jamaa huyo naye akigeuka mbogo huku akijaribu kujitetea na kuwa mkali bila mafanikio.

No comments:

Post a Comment

SUFIANIMAFOTO Copyright © 2014

Theme images by Bim. Powered by Blogger.