MICHUANO ya 29 ya Kombe la Mataifa Afrika, imemalizika jana usiku kwa timu ya Nigeria kuibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Burkina Faso, mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Soccer City.
Nigeria ilitinga fainali hizo na Burkina Faso inayofanana na ya mwaka jana, ambapo timu iliyokuwa ikipewa nafasi ya kutwaa ubingwa huo zaidi ilikuwa ni (Ivory Coast) ambayo ililala kwa mikwaju ya penati dhidi ya timu iliyokuwa ikidharauliwa zaidi (Zambia).
Tofauti na mwaka jana ambapo bingwa alipatikana baada ya dakika 120, kwa mikwaju ya penati.
Toka awali Nigeria ilipewa nafasi kubwa ya kutwaa ubingwa wa tatu wa fainali hizo, baada ya kufanya hivyo katika miaka ya 1980 na 1994 na huu wa mwaka huu wa 2013 licha ya ukweli kuwa hiyo ni fainali yao ya kwanza tangu 2000 walipokubali kichapo mbele ya ‘Simba Wasioshindika’ Cameroon.
TUJIKUMBUSHE:-
Nigeria na Burkina Faso zilikuwa katika kundi la C, ambalo walipoukutana katika mechi baina yao walitoka sare ya 1-1, ambapo Super Eagle ilitangulia kufunga dakika ya 23 kupitia Emmanuel Emenike, kabla ya Burkina kuchomoa dakika ya 90 kupitia Alain Traore.
Emenike ambaye ni kinara wa mabao amemaliza mechi hizo akiwa na jumla ya mabao 4, alikuwa ni sehemu ya kikosi cha Nigeria, huku Traore wa Burkina mwenye mabao matatu akiwa majeruhi, ingawa nafasi yake ilichukuliwa na Jonathan Pitroipa – aliyefutiwa kadi nyekundu.
Katika robo fainali ya michuano hiyo, Burkina Faso iliichapa Togo kwa bao 1-0 katika pambano la dakika 120, kabla ya kuing’oa Ghana kwa matuta katika nusu fainali – baada ya sare ya bao 1-1 ya dakika 120 za pambano hilo lililoharibiwa na mwamuzi Slim Jdidi.
Kwa upande wao Nigeria katika robo fainali waliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya timu iliyokuwa ikipewa nafasi kubwa ya kufika fainali ya Ivory Coast, kisha ikaja kushinda nusu fainali kwa ushindi wa kishindo wa mabao 4-1 dhidi ya Mali.
|
No comments:
Post a Comment