Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitoa heshima za Mwisho mbele ya jeneza la Askofu Mtsaafu jimbo Katoliki la Moshi Marehemu Mhashamu Amedeus Msarikie wakati wa misa ya Mazishi iliyofanyika katika kanisa na Kristu Mfalme, mjini Moshi leo.
Rais wa Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, leo Alhamisi, Februari 14, 2013 ameungana na mamia kwa mamia ya waumini wa Kanisa Katoliki, Jimbo la Moshi na kutoka sehemu nyingine nchini, kumzika Askofu Mstahivu (Bishop Emeritus) Amedeus Peter Msarikie.
|
Rais Kikwete amewasili kwenye Kanisa Kuu la
Kristo Mfalme mjini Moshi kiasi cha saa sita na dakika tano mchana kuungana na
marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi na Benjamin Mkapa na mamia kwa mamia wananchi
kwa ajili ya mazishi ya Askofu Msarikie ambaye alifariki dunia Alhamisi
iliyopita, Februari 7, 2013 kwa ugonjwa wa saratani katika hospitali moja mjini
Nairobi, Kenya.
Mara baada ya
kuwasili, Rais Kikwete ametia saini kwenye kitabu cha maombolezo na ikaanza
ibada ya mazishi ilivyohudhuriwa na mamia kwa mamia ya wananchi wakiwamo
maaskofu zaidi ya 20 kutoka majimbo mbali mbali ya Kanisa Katoliki nchini.
Mwili wa Marehemu
Msarikie uliteremshwa kaburini kiasi cha saa saba na dakika 35 ndani ya Kanisa
hilo na Rais Kikwete akaweka udogo kwenye kaburi na baadaye shada la maua.
Akizungumza kwenye
mazishi hayo, Rais Kikwete amemwelezea Askofu Msarikie ambaye alikuwa Askofu wa
Jimbo la Moshi kwa miaka 26 kama “kiongozi shupavu wa kiroho ambaye aliwalea
vyema kondoo wa bwana. Lakini pia alikuwa kiongozi hodari kwa maendeleo ya
jamii yaliyowanufaisha waumini wake na hata wale wa madhehebu na dini
nyingine.”
Amesisitiza Rais
Kikwete: “Kwa kweli sote tumepoteza mtu muhimu. Tunamfahamu marehemu Baba
Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowatendea watu wa jimbo lake, ya kiroho na
ya maendeleo. Mimi binafsi, wana-moshi na Watanzania kwa ujumla tutamkumbuka na
kumuenzi Baba Askofu Msarikie kwa mema mengi aliyowafanya wanadamu wenzake na
nchi yetu.”
No comments:
Post a Comment